Sunday, September 9, 2012
TUNAENDELEA KUWEKEZA AMERIKA YA KUSINI..
Mfalme wa makocha duniani,Sir Alex Ferguson amesema wameamua kupanua shughuli zao za kutafuta wachezaji katika bara la Amerika ya Kusini,hii inafuatia baada ya hivi karibuni kumnyakua kinda wa Chile Angelo Henriquez..
''Kusema ukweli wanazalisha,bara la Amerika ya Kusini wanapenda mpira sana,nadhani iko kwenye damu yao,hata Manchester United wale wabrazil watatu huwa wakwanza kuwasili mazoezini(Fabio,Rafael na Anderson) ni kitu wanachopenda kufanya'' Ferguson akiongea na tovuti ya Manchester United.
''Shughuli zetu kule zimeongezeka sasa,tuna ofisi Mexico,scout wawili Brazil na wengine wanne bara zima,ukimuangalia mtu kama Valencia,mgumu kama msumari pamoja na nidhamu ya hali ya juu pia heshima aliyo nayo Chicharito na uwezo wake,tumefanya kazi kubwa sana eneo hilo la dunia ndani ya miaka 2-3 iliyopita''
Aliendelea kusema Ferguson.
Man United sasa inajivunia idadi ya wachezaji sita kutoka ukanda huo wa dunia,Fabio(aliyepelekwa kwa mkopo QPR),Rafael,Valencia,Anderson,Henriquez na Chicharito. Wote hawa wakiwa kwenye kikosi cha kwanza.
Labels:
Anderson,
Angelo Henriquez,
Chicharito,
Fabio,
Rafael,
Valencia
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment