Ads 468x60px

Monday, September 10, 2012

MAN UTD KUINGIA VITANI ILI KUMRUDISHA CR7 OLD TRAFFORD

FUNUNU/TETESI.




Habari za chini kwa chini zinaeleza kuwa Ferguson yuko mbioni kugonga hodi kwa wamiliki wa club na kudai fungu la kumrudisha kundini CR7,hii inafuatia tukio la hivi karibuni baada ya Ronaldo kufunga goli na kuacha kushangilia,alipoulizwa kwa nini hakushangilia alikuwa mwepesi kusema ''sina furaha Real Madrid,na uongozi unajua kwa nini sina furaha hapa'' baada ya kauli hiyo kila mtu akawa na lake la kuongea huku wengine wakihusisha na suala la kudai nyongeza ya mshahara itakayofuatia baada ya kutia saini mkataba mpya,kiasi hicho ambacho inasemekana Real Madrid hawako tayari kuifikia ni fungu la £500 kwa wiki!!
Ronaldo anadai kiasi hicho ili aepuke mtikisiko wa uchumi unaoikumba taifa la Hispani ambayo serikali imeamua kuongeza kodi kwa wale wafanyakazi wanaolipwa kiasi cha kuanzia £100,000 kwa wiki.

Kumrudisha Ronaldo Man United itagharimu kiasi cha £100m za uhamisho mbali na mshahara wa £500,000 atakaokuwa anadai kila wiki,inaaminika kuwa tukio hili likitokea litasababisha wachezaji wengi wa Man Utd kudai ongezeko la mshahara pia!

Upande mwingine wa watu wa karibu wa mchezaji huyo aliyewahi kung'ara na mashetani wekundu hadi kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa dunia unadai kuwa kinachomkosesha raha CR7 ni dharau kutoka kwa wachezaji wenzake,pia wanadhani Ronaldo hapewi heshima anayostahili kutokana na kiwango alichoonyesha miaka 3 iliyopita! Ronaldo amefanikiwa kutikisa nyavu mara 150 katika mechi 149 alizocheza za Real Madrid! wastani wa goli moja kila mechi!!!

0 comments:

Post a Comment