Ads 468x60px

Thursday, January 24, 2013

Giggs,The New United Coach???

Habari zenu wadau..
Naomba nishirikiane na nyie kwenye hili,ni mawazo yangu binafsi najaribu kuchanganya picha ili nipate moja kubwa,nzuri na yenye muonekano halisi! Unayo ruhusa ya kuchangia kwa kupinga au kuongezea kitu..

KWANINI FERGUSON BADO ANA KAMA 3 OR 2 YEARS ZA KUFUNDISHA PALE OLD TRAFFORD NA NANI NAHISI ATAMRITHI.


1.Pep Guardiola
Hii ni sababu ya kwanza inayonipa kiburi cha kusema Ferguson bado tunaye,mwanzoni nilijiaminisha kama wenzangu kuwa huyu ndo mtu anayesubiri kupokea mikoba ya babu pale hasa ukizingatia style yake ya kufundisha inayothamini wachezaji wazawa na mchanganyiko kidogo wa ugenini ukiweka na kuwa ni mtu aliye na utayari wa kukaa kwenye club moja kwa muda mrefu kidogo kulinganisha na wengine! Baada ya kutangazwa rasmi kuwa anatua Bayern Munich sasa naamini SAF bado yuko pale Old Trafford.


2.David Moyes
Huyu ni kocha wa Everton ambaye wachambuzi mbali mbali wamekuwa wakimfananisha na Ferguson kwa kusema kuwa ana system ya uongozi nzuri kama ya babu kuanzia staff wa kawaida hadi uwanjani,wote wanakuwa wanamuangalia kama nyota ya team,ana uwezo binafsi wa kucontroll wachezaji nyota wasilete matatizo kwenye club na pia ni raia wa Scotland anapotoka SAF.
Hivi juzi kumekuwa na taarifa zinazosema kuwa huenda Chelsea wakamchukua yeye baada ya kumaliza list ya makocha wakubwa na ukizingatia matatizo ya mastaa pale Stamford wanaamini huyu ndo mwarobaini wao.Hili bado linazidi kunipa moyo kuwa bado tunaye babu sana.


3.Mourinho
Huyu tangu mwanzo namkubali kwa uwezo wake lakini tabia yake ya kubeba kobe na kukimbia haitamruhusu afunguliwe milango ya ukocha pale Old Trafford,United sio team ya kuhangaika kutafuta makocha kila mwisho wa msimu au miwili. Huyu nilijua na bado nahisi hatoweza kupewa ruhusa ya kuja pale.Sababu nyingine ya kwanini babu anaendelea kuwa kocha pale.

4.Usajili wa Wilfried Zaha
Endapo ndani ya masaa machache yajayo atatangazwa huyu kijana kutua Old Trafford basi inaniaminisha kuwa Babu kamchukua na ameamua kumuhangaikia kwa kuwa ana mpango naye,na kama ana mpango naye kwanini aondoke mwisho wa msimu? Babu bado tunaye pale Old Trafford kwa hii issue ya Zaha

5.Ryan Giggs na badge za ukocha
Hivi karibuni imefahamika kuwa Giggs atakuwa mchezaji wa kwanza kupewa ''leseni za awali'' za kufundisha huku akiwa mchezaji bado,hii inaniambia kuwa huyu kijana anapikwa chini kwa chini na Babu na hilo linatupeleka hadi misimu miwili au mitatu ijayo ambayo Babu atahakikisha amemuacha Giggs na kila kitu cha kuweza kutuongoza pale Old Trafford



CONCLUSION:
Nikijaribu kuunganisha picha zote hizo nagundua kuwa babu bado tunaye sana na kitu kinachombakiza ni kuhakikisha anamuacha Giggs katika kiti salama cha ukocha,baada ya kusema hivyo naomba niseme kuwa Giggs ndo kocha anyemrithi babu pale Old Trafford,hili litawashangaza sana watu!!! Ila ndo picha inapoelekea. Ukizingatia Giggs ni mchezaji aliyekaa pale toka '92 anayeijua timu vizuri na jinsi inavyoendeshwa.

Unaweza Kuongeza Au Kupinga Kwa Hoja..Karibu.

1 comments:

Wawila said...

Kaka Steve mimi naitwa Wawila Mwazembe ManU ni wangu toka muda mrefu sana. Naweza kukubaliana nawe kuhusiana na Ryan Giggs ingawa babu mwenyewe kipindi cha nyuma alionyesha kutaka kumuachia hiyo nafasi Gary Neville.Toka 92 mpaka sasa Giggs anajua nini hasa kifanyike katika timu yake kama kocha vilevile ni MUFC ni timu ambayo haikubali/haitaweza kukubali kukaa mwaka 1 au 2 kupita bila kikombe. kwahiyo naona Ryan Giggs siye ambaye babu anamfikiria kwa sasa baada ya miaka 3 ijayo.Mtu ambaye ataendelea kutoa ushindani kwa wachezaji wawe wakubwa kwa wadogo,kucontrol usumbufu SAF tunaye kwa kipindi hicho unachosema cha miaka 3 mingine.
alivyongea kwa rafiki wake wa karibu sana Marcelo Lippi inaonekana mikoba yote bado anata kumuachia Guadiola baada ya miaka 3 ndo anamini ndo ataiweza united.

Post a Comment