Ads 468x60px

Tuesday, September 11, 2012

Mifumo 5 Man United Itakayoweza Kuitumia Msimu Huu

Kagawa,RvP,Rooney,Valencia,Nani,Vidic,Ferdinand..unawatumiaje hawa watu msimuu huu??




4-4-2


Kwa hali iliyoko sasa kila mtu anaamini kuwa Kagawa bado hajaanza kutumiwa ipasavyo kama ilivyokuwa na team yake Dortmund huko Ujerumani,na mfumo huu ndiyo utaharibu kabisa,japo ni mfumo utakaofanya ''wakali wanne'' wa Man United wote waanze na pia bila kusahau ni mfumo uliotumika kwa miaka kadhaa sasa kuiletea Manchester United ubingwa na mafanikio mbali mbali lakini iwe wazi kuwa kumchezesha Rooney na RvP mbele sio kitu atakachotaka au kuweza RvP,kwa miaka mingi RvP anapendelea na ni moto akicheza kama ''mshambuliaji mpweke'' mbele na pia hii itazidi kumzuia Kagawa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji kwani itamvuta kati na kufanya asimame na Carrick au Scholes kwenye kukaba huku akiweka kichwani kuwa Rooney na RvP ndiyo watu wa kwanza kushambulia zikifuatia na winga mbili(kulia na kushoto) halafu ndiyo aje yeye wa mwisho

4-2-3-1


Hii inaonekana kama ina mafanikio lakini itamzuia Ferguson kuingiza wachezaji nyota wake wote,RvP atasimama mbele kama inavyotakiwa lakini itasababisha Rooney apiganie nafasi na RvP au Kagawa,tofauti na 4-3-3 ni kwamba hii inaondoa umuhimu wa Tom Cleverly kwa kuongeza kiungo mkabaji mmoja hapo katikati na ambayo kwa inavyoonekana anaweza kucheza Jones na Carrick

4-3-3


Hii imesaidia kwa mechi hizi za mwanzo msimu huu,mbinu hii inamuweka RvP mbele peke yake na hadi sasa tumeshuhudia RvP akifunga goli 4 katika mechi 3 kutokana na mbinu hii,sema sasa inamuweka Rooney pabaya,pamoja na kuwa Rooney anaweza kubadilika na kucheza popote lakini swali ni je atamtoa mtu gani kwenye nafasi yake ya asili?Uwezo wa kucheza nafasi ya Valencia anao lakini ukweli ni kuwa Valencia ni mmoja ya watu muhimu sana kwenye ile nafasi dunia ya leo,na je kwa Carrick?hapana pia..bado tunamuhitaji mtu kama Carrick pale katikati,hii itafanya Rooney aonje benchi mara moja  moja akipokezana na Kagawa.

4-5-1 au 3-6-1


Hii tena inaleta nyota wote wa United pamoja,inaua beki mmoja kati ya wanne wa mwisho na kuzalisha kazi mara mbili kwa mawinga,kila nyota atacheza nafasi aliyoizoea pale mbele,RvP atabaki peke yake kama kawaida,Rooney atacheza na Kagawa pembeni yake na shimoni katikati Jones na Carrick watatawala.
Hii itafanya mawinga wawe na kazi mara mbili,za kushambulia na kukaba,kwa kusimamisha milingoti mitatu nyuma ina maanisha kuwa winga za kulia na kushoto zitahitajika pia kurudi nyuma na kucheza namba mbili na tatu,hii inatia hamu ya kuona wakicheza kwani kwenye makaratasi inaonyesha kama inazaliasha goli 3-4 kwa kila mechi

3-4-3


Hii inaonekana ni mahususi kwa ajili ya kusaidia ukuta wa kukaba wa Man United,Kagawa anarudi shimoni na winga zote mbili zitahitajika zicheze kama beki na winga,itawachosha sana ila itasaidia kukaba LAKINI itambulike kuwa Manchester United siyo Chelsea,hawatataka kucheza mchezo wa kukaba kila saa kwa hio hii inaweza kutumika mara moja moja kwenye mechi ngumu tu.

0 comments:

Post a Comment