Kufuatia taarifa zilizosambaa kwenye mtandao kuwa mashine mbili mpya na tegemezi za Manchester United zimeumia zikiwa kwenye majukumu yao ya taifa,taarifa tulizozipata sasa ni kuwa wote wawili ni hawana matatizo ya kuwafanya wakose mechi zijazo ukianza na ya wiki hii dhidi ya Wigan nyumbani Old Trafford.
Tukianza na Robin Van Persie aliyetolewa mapumziko na kocha wa Uholanzi,kocha huyo( Louis van Gaal ) amesema ''hamna cha kuogopesha,nimemtoa tu kama tahadhari''
Huku kwa Mjapan,kiungo mshambuliaji Shinji Kagawa aliyeachwa kwenye kikosi cha kwanza kilichocheza dhidi ya Iraq,Chama cha soka cha Japan kimeliambia gazeti la daily sports kuwa ''alikuwa akijiskia maumivu kidogo kwenye mgongoni akiwa anafanya mazoezi,tukasema tusubiri siku moja tuone itakuwa vipi,lakini hayuko fiti 100%,so tukamuacha,na hajaenda hospitali''
Huku Kagawa mwenyewe akisema ''maumivu yalianza jana mazoezini,nilikuwa na mpira najiandaa kuupiga hapo ndiyo maumivu yakanianza mgongoni,ila haitanichukua muda mrefu kupona''
Blog hii inawapa pole RvP na Kagawa,Mungu awaponye warudi mapema uwanjani.
Tuesday, September 11, 2012
Kocha akataa RVP kupata jeraha,Kagawa naye asema yuko fiti
Labels:
Manchester United,
Robin Van Persie,
Shinji Kagawa
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment