Saturday, December 29, 2012
Sir Alex Ferguson - Alan Pardew Is A Hypocrite(VIDEO)
Friday, December 28, 2012
ADMIN WA MWAKA(KATIKA PAGE)
HII NDIYO ILE KUBWA, Katika hili hatujaangalia admin gani yuko active sana. Ila tumeangalia aliyetufanya tukutane hapa, tuwe pamoja na kuleta mkusanyiko huu.
ADMIN OF THE YEAR niiiiiiiiiiiii DERICK LAWRENCE(Kwa Heshima Kubwa).
Bila Kumsahau Stephen M. Beda(Red Steph) kwa ushauri Mkubwa wa kuendeleza page hii, Na MaAdmin wengine.
PAZIA LA MWAKA 2012 TUMELIFUNGA #GGMU
Labels:
Admin Of The Year
FAN WA MWAKA, TOP FAN(FACEBOOK PAGE)
Labels:
Fan Of The Year
TOP 10 FANS TZ. (FACEBOOK OFFICIAL PAGE)
Haaaya Sasa Huu Ndo Mda!! Hii ni TOP 10 FANS WA MWAKA 2012. Hawa wametoa Mchango wote kwa Pamoja
1. Mohamed Hassan Mazoa
2. Omari Kagawa Bobani
3. Princess Johari De Sagirio
4. Eddy Kudoha
5. Abdul van Mwasha.
6. Gabriel Majaliwa
7. Amos C. Belege
8. Ceaser Mtangi
9. Feed Mkama Paschal
10. WOTE AMBAO HATUJAWATAJA MMETOA MCHANGO MKUBWA
MWAKA 2012
#GGMU
Labels:
Top 10 Fans Of The Year
Tuesday, December 25, 2012
MANCHESTER UNITED CHRISTMAS CHALLENGE(ONA VITUKO VYA EVRA NA QUINTONE FORTUNE)
Players vs. Legends vs. Coaches -- all in the name of fun!
Players - Patrice Evra, David De Gea, Darren Fletcher
Coaches - Tony Strudwick, Richard Hawkins, Rene Meuelensteen
Legends - Mickey Thomas, Bryan Robson, Quinton Fortune
Manchester United Christmas Challenge 2012
Saturday, December 22, 2012
Swansea vs Man United-PREVIEW
Viongozi wa ligi weekend hii wanasafiri nje kidogo ya Uingereza,wanaingia nchini Wales kupambana na vijana wanaosadikika kuwa wamechukua sifa ya Arsenal ya kucheza mpira safi na wenye kuvutia,vijana hao sio wengine bali ni Swansea ama ''Swanselona'' kama mashabiki wanavyowaita.
Swansea wamekuwa ni nyoka wenye sumu kali sana hasa wanavyokutana na timu kubwa,wanaongeza umakini kwenye mechi na hayo yoyte yanatetea na mtu mmoja tu,mshambuliaji wao hataaaari asiye na huruma na nyavu MICHU!
Upande wa pili wa shilingi unaowazungumzia wageni ambao ni vinara wa ligi kwa tofauti ya point 6,Man United una sumu kali mara mbili ya hawa wanaoitwa Swanselona.ujio wa Robin Van Persie kutoka Arsenal umeongeza sumu ya United huku akisaidiwa na striker mwenzake mwenye uwezo wa kucheza namba yoyote uwanjani(hata golikipa) Wayne ''Wazzaaa'' Rooney.
Rooney na Van Persie msimu huu wameanza pamoja mara 12 na mechi zote hizo United kashinda zote. Inasadikika pacha yao ndo pacha hatari kwa sasa ligi kuu ukizingatia Robin Van Persie yuko pale juu akiminyana na Michu kwa idadi ya magoli kumi na mbili kila mmoja.
VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA KWENYE HII MECHI
*Mara ya mwisho Swansea wanashinda mechi ya nyumbani dhidi ya Man United ilikuwa Januari 1982
*Swansea wamefunga goli moja tu kutoka kwenye mipira iliyokufa msimu huu,mengine yote yaliyobaki 25 wamefunga kwenye mchezo wa pasi
*Hadi sasa Man United magoli yake yamefungwa na wachezaji 15 tofauti
*Man United wanaongoza kwa magoli ya krosi (14) msimu huu na pia wanaongoza kwa magoli ya vichwa(10) msimu huu
WACHEZAJI WA KUWAANGALIA
SWANSEA.
MICHU
Umakini wake na njaa yake ya magoli haufanani na pesa kidogo aliyonunuliwa £2m
Ni hatari sana hasa kama United wataendelea na mchezo wa mabeki wake kujisahau
Ana magoli 12 katika game 17 alizoanza,huku akifunga 6 katika michezo yake 6 ya mwisho
MAN UTD
ROBIN VAN PERSIE
Kwa baadhi ya amshabiki wa United ni kama bado wako kwenye ndoto,hawaamini kama huyu muuaji amekubali kutua Old Trafford kutokea Arsenal,ameisaidia sana na kuitoa Man United shimoni msimu huu
Ni kinara wa magoli pamoja na Michu wote wakiwa na magoli 12 pale juu
MAJERUHI
Man United bado itaendelea kuwakosa Luis Nani,RafaelAnderson,Kagawa huku Vidic akipatikana lakini kuwa na uwezekano mdogo wa kuanza hii mechi. Evans na yeye amepona na kwa taarifa kutoka kwa kocha ni kuwa anaweza kucheza.

Manchester United,
Michu,
Robin Van Persie,
Rooney,
Swansea,
Wales
Sunday, December 16, 2012
PEP GUARDIOLA NDIYE MTU SAHIHI KWA TIMU YETU
Kwanini nadhani Manchester United ni nyumbani au panamfaa Pep Guardiola kuliko City,Chelsea au Arsenal!
Katika ulimwengu wa sasa sidhani kama kuna hesabu rahisi kama Kocha Mpya + Chelsea=?
Moja kwa moja jibu ni ''Kufukuzwa wakati wowote'',hesabu zingekuwa hivi tusingekuwa tunafeli wengine hapa!
Baada ya Pep kuachia ngazi Barca na kusema kuwa atapumzika kwa mwaka mzima bila kufundisha Chelsea walitumia mwanya huu kuanza kumtongoza na pesa zao,ukizingatia Pep alishatamka kuwa

angefurahi siku kuwafundisha Mata,Oscar na Hazard,Chelsea wakatuma
maombi kwa mara ya kwanza,yakagonga mwamba..wakasubiri,huku Pep
akiendelea kuifuatilia Chelsea kwa kutia maneno ''Chelsea wamejengeka
vizuri sana msimu huu,nimependa walivyoanza'' Na kweli bila
hiyana,Chelsea walianza kwa moto sana,lakini ghafla bin vu Di Matteo
akatimuliwa,pesa za Abromivich zikamtuma kuwa Pep ndo mtu wa kuja kujaza
hiyo nafasi lakini akaumbuka Pesa sio kila kitu,pesa haiwezi kumfanya
Messi akacheze Man City na pesa pia haiwezi kumfanya Ferguson astaafu
Man United na kwenda China hata kwa £1b kwa mwaka
October Chelsea wakagonga mwamba tena!
KWANINI MAN UNITED KUNAMFAA?
1.Uhakika wa kukaa kazini kwa muda mrefu
Hili halihitaji maelezo,tumeshuhudia Ferguson akaikaa kazini zaidi ya umri wa wengi wetu huku ndani,wangapi walikua wamezaliwa 86??Ferguson ndo anaanza kazi ya United hapo! Sisemi Pep anatafuta team ya kukaa miaka 26,hapana,ila ni mtu anayetaka team itakayompa muda wa kufanya mambo yake! sio kutimuana kama boss na housegirl
2.Enough resources
Wengi wanaweza kubisha juu ya hili lakini sina maana ya kuwa tuna pesa za kumwaga kama Man City au Chelsea,ndio sisi ni club tajiri lakini hatuna mmiliki tajiri ila kiasi chochote anachotaka kocha anapewa kwa ajili ya maendeleo ya team,hili naomba nithibitishe kwa kauli waliyotoa Glazer Family kuwa Ferguson hata akitaka kumrudisha Ronaldo,pesa iko!!
Kupitia hili ndahani Pep atakuwa na jeuri ya kufanya kazi katika mazingira mazuri pamoja na vitendea azi vya kutosha
3.Barcelona ni kama Man United
Angalia mnavyoshangaa..sijasema tunacheza mchezo wa aina moja(msije mkanitoa roho kwa kuandika uwongo)
Barcelona ni ''football family'' na ndivyo ilivyo wa Man United pia,wiki chache zilizopita Barcelona ilivyocheza na Levante ilikuwa na wachezaji wote 11 kutoka kwenye Academy yao
Man United nasi hatuko mbali sana kwenye hilo,Welbeck,Cleverly,Giggs na Scholes hao ni tunaowajua ila kutokana na takwimu zilizotoka juzi kuwa United ni club ya tano duniani na ya kwanza Uingereza kwa academies bora basi hapa ndo nyumbani kwa Pep. Man City bila ya kumchezesha Miccah Richards basi hawana mchezaji aliyekulia pale,Chelsea nao hivyo hivyo hola!
Baada ya kusema hayo;
Kwanini sio
Cheslea? Atatimuliwa mapema na hayuko tayari kuchafua CV pale
Man City? Hajazoea kufanya kazi kwenye mazingira ya kifahari hivyo bila kuwa na watu wanaopigania team(wazawa)
Arsenal? Hawana pesa ya kumlipa kama mshara na pia hawatampa kiasi cha kutosha kwenye kununua vitendea kazi
Kwanini Mourinho hawezi kufundisha Man United?
Mtanisamehe kwa hili neno lakini Mourinho ni kocha ''MALAYA''
Ni kocha mzuri sana,japo wengi wetu hatujui kuwa kinachombeba Mourinho ni Man Management na sio skills,ourinho anaweza akakujaza moyo na kukuaminisha kuwa '''bila ya wewe Welbeck Man United Sio Kitu''' ni mzuri sana ila sio wa kukaa sana kwenye club,ndiyo tunahitaji mtu wa kukaa,hatujazoea kubadilisha ovyo,atakuja abebe makombe mawili ya ligi halafu aseme ''I'm looking for Challenges elsewhere''
KUNA MTU YOYOTE ANA MAONI TOFAUTI NA HAYA YANGU KWENYE HILI?NIKO TAYARI KUSAHIHISHWA

Pep Guardiola
Saturday, December 8, 2012
DERBY DAY: MATCH PREVIEW
Pre Match
December 9, 2012
Etihad Stadium — Manchester
Referee: M. Atkinson
December 9, 2012
Etihad Stadium — Manchester
Referee: M. Atkinson
Manchester City - Manchester United Preview: Rivals clash in table-topping tie
Sir Alex Ferguson's side go to the Etihad three points clear of Roberto Mancini's Premier League champions, who will want to pick themselves up after a dismal Champions League exit
SOMA ZAIDI>> http://www.goal.com/en/match/80976/manchester-city-fc-vs-man-utd/preview
Labels:
Manchester City
HII SI YA KUKOSA: vs MAN CITY @eTIHAD (DERBY DAY)
Labels:
Manchester City,
Manchester United
Wednesday, November 28, 2012
KUELEKEA MCHEZO WA LEO USIKU DHIDI YA WEST HAM
Man United usiku wa leo inawakaribisha vijana waliopanda daraja msimu huu WEST HAM UNITED wanaoshikilia nafasi ya 8 kwenye ligi hadi sasa.
MANCHESTER UNITED
Michezo 5 ya mwisho W W L W W
Mchezo wa mwisho Man Utd 3-1 QPR
WEST HAM UNITED
Michezo 5 ya mwisho L D W D L
Mchezo wa mwisho Tottenham 3- 1 West Ham
Kagawa anaweza kucheza baada ya kufanikiwa kupona,Nani na Vidic bado ni majeruhi pamoja na Valencia. Kama alivyosema Ferguson,Anderson ataanza mchezo na West Ham baada ya kucheza vizuri mechi iliyopita dhidi ya QPR.
Matatizo yanayoikumba Man Utd ya mabeki yanaweza kuwa yameisha baada ya uhakika wa kuwepo kwa Rio Ferdinand,Evans,Smallin na Jones huku Scholes akiwa kwenye adhabu baada ya kupokea kadi yake ya 5 ya njano dhidi ya QPR mechi iliyopita.

Anderson,
Evans,
Kagawa,
Man Utd,
Old Trafford,
Rio Ferdinand,
Scholes,
Smalling,
West Ham
HATIMAYE KITABU CHA MAISHA YA WACHEZAJI WA MAN UTD ''SONS OF UNITED'' CHAKAMILIKA
Hatimaye kile kitabu kilichotumia miaka 18,kilichoandikwa na mfanyabiashara wa Droitwich Spa kimekamilika..
Kitabu hicho kinachoelezea kwa kina maisha ya makinda wa Man Utd kuanzia wakiwa wadogo na mahojiano pamoja na picha kiko sokoni,Steve Hobin amefanya mahojiano na wachezaji wengi kwenye kitabu hicho kuanzia Bobby Charlton,Ryan Giggs,Beckham na Scholes kimeshaanza kununuliwa kupitia internet ulimwenguni kote.
Kitabu hicho kina kurasa 576 na kimechapisha nakala 2,000 tu!
Kitabu hicho kinachoelezea kwa kina maisha ya makinda wa Man Utd kuanzia wakiwa wadogo na mahojiano pamoja na picha kiko sokoni,Steve Hobin amefanya mahojiano na wachezaji wengi kwenye kitabu hicho kuanzia Bobby Charlton,Ryan Giggs,Beckham na Scholes kimeshaanza kununuliwa kupitia internet ulimwenguni kote.
Tuesday, November 27, 2012
TAARABT KUTUA OLD TRAFFORD????
Kiungo mchezeshaji wa Morroco Adel Taarabt anaweza kutua Old Trafford January hii,hii inatokana na kuwasili kwa kocha mpya QPR Harry Redknapp,hapo mwanzo wakati anatoka Lens na kutua Tottenham
alibeba matumaini ya watu wengi huku wengine wakidiriki kumuita ''Zidane Mpya'',hakuwa na mahusiano mazuri na Harry Redknapp hadi kupelekea kuuzwa QPR na kocha huyo,sasa kocha huyo kamwaga wino QPR kuna uwezekano wa kiungo huyo kutua Old Trafford kwani amekuwa kwenye akili ya Babu kwa muda sasa.

Harry Redknapp,
Morroco,
QPR,
Taarabt
CLEVERLEY KUFUNGWA PINGU OLD TRAFFORD
Baadhi ya wachambuzi wa soka wameshaanza kumvisha majukumu mazito kwa kumfananisha na Paul Scholes,kiungo huyu kinda wa Man Utd anatarajia kupewa mkataba wa muda mrefu ifikapo mwaka mpya.
Kwa sasa Cleverley mkataba wake ni £35,000 hivyo anatarajia kutia saini mkataba wa miaka mitano utakaofanya alipwe sasa £60,000 kwa wiki!
Kiwango chake kwa sasa hakijamuwezesha kukaa chini na kujadili mkataba mpya,bali hata kupata namba ya uhakika kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza!
Babu anatarajia kuwapa mikataba ya kifungo kirefu wachezaji wake wote wadogo kama njia ya kutengeneza misingi ya baadae ya klabu,wengine walioko kwenye hatua hiyo ni Smalling,Jones na Chicharito.

Cleverley,
Javier Hernandez Chicharito,
Jones,
Smalling
ASHLEY YOUNG,UVUMILIVU UNATUSHINDA!
Wakati Boss anaenda kumwaga £17M kumnunua Young watu wengi walishtuka kidogo,tulikuwa bado tuna uwezo wa kuwachezesha Rooney,Welbeck na Luis Nani upande ule wa kushoto(kama tatizo lilikuwa ni mtu wa kucheza kushoto) Kuongezea hilo bado tulikuwa na Fabio na Giggs ambao wangeweza kuokoa hiyo pesa iliyoenda kwa Young!! Hatusemi tumenunua plastiki,la hasha ila maisha ya uwezo wa Young yalidumu kwa muda wa miezi mitatu tu ya mwanzo,baada ya hapo kama sio majeraha basi itakuwa ni kucheza chini ya kiwango,matatizo baada ya matatizo!
Nadiriki kusema timu ya ''scouting'' ilifanya mahesabu mabaya,ni muda huo huo mashabiki tulikua tunatarajia babu atanunua wachezaji 2 au 1 kwenye nafasi ya kiungo mkabaji,lakini matarajio yetu yakawa ndivyo sivyo,akaja kijana mwingine kujaza kontena la mawinga tulionao.
Sisemi Young ni mchezaji mbaya kiasi cha kufikia hatua ya kumfananisha na Bebe,hapana. Msimu wake wa kwanza United alitupa magoli 6 na Assists 9,sio mbaya kwa winga..lakini ni mbaya kwa winga wa £17M aliyerekodi assists 17 msimu wake wa kwanza Aston Villa na Assists 14 msimu wa mwisho kabla hajasajiliwa Man United.
Kwa hali ilivyo sasa, majeruhi Nani na Kagawa wakipona tutaanza kusahau uwepo wa Young,hasa pale babu akiamua kutumia mfumo wa ''diamond'' 4-3-3 uliotuletea mafanikio makubwa dhidi ya Braga na New Castle msimu huu.
Valencia anaweza kuwa kwenye form mbovu msimu huu lakini bado ana uwezo wa kulaza mabeki wawili au watatu na kulazimisha krosi ndani.
NI WAKATI WA YOUNG KUTHIBITISHA KUWA HATUKUFANYA MAKOSA KUONGEZA WINGA WAKATI TUNA MATATIZO YA KIUNGO MKABAJI,HILI LINAWEZA LIKAWA MZIGO NA MTIHANI KWAKE LAKINI MWISHO WA SIKU ANALIPWA ILI AFANYE HII KAZI.
Monday, November 26, 2012
MAAMUZI MATANO (5) YA KIUFUNDI YATAKAYOTUSAIDIA KUBEBA KOMBE LA 20
ZIFAHAMU NJIA TANO ALIZOTOA MMOJA WA MASHABIKI WA MAN UTD KUELEKEA KOMBE LA 20.
Baada ya Chelsea na City kudroo mechi yao na sisi kurudi kileleni ,tena baada ya kupoteza michezo mitatu katika 13 tuliyocheza hadi sasa ni dhahiri kuwa taji la 20 sio shida kulibeba,endapo tutafanya mmamuzi haya matano ya kiufundi yatakayoweza kutusaidia kubeba ndoo ya 20.
1.GIGGS & SCHOLES WAAGE SASA NA KUONDOKA KWA AMANI.
Nawapenda sana hawa maveterani wa soka na wameisaidia United katika kila namna hadi tumefikia hapa tulipo leo.
Baada ya kutizama mechi zetu mbili dhidi ya QPR na NORWICH na kuona jinsi hawa maveterani wanavyotaabika katikati na ukizingatia sio dhidi ya Barcelona au Madri basi utakubaliana na mimi kuwa wakati umeshawatupa mkono.Wnahitaji kustaafu kwa heshima,tuna wachezaji wengi na wazuri zaidi yao katika hilo eneo,ni muda sasa wawapishe damu changa wafanye kazi.
2. DAVID DE GEA ACHEZE KILA MCHEZO WA ''LIGI KUU''
Nafahamu kuwa alikuwa anaumwa na hakuweza kucheza dhidi ya Norwich lakini De Gea alitakiwa awepo golini katika mechi dhidi ya QPR,uwepo wake kabla ya Anderson kuja kunyanyua team ungetusaidia sana.De Gea anafanya kazi ambayo Lindegaard yeye kwake ni ndoto kuifanya,hawezi kufikia kiwango cha De Gea. De Gea ametuokoa sana na kutubeba msimu uliopita hadi kufikia kupoteza kombe kwa tofauti ya magoli.
Huu ni muda wa Ferguson kulazimisha huyu aanze kila mchezo wa ligi kuu.
3.ACHA KUMCHEZESHA WELBECK PEMBENI
Hili ni somo ambalo liko wazi sana kwa kila mtu kuona.England ni mwalimu wetu kwenye hili somo,Danny amekuwa kwenye form akicheza na team ya taifa kwa kuwa anachezeshwa katika nafasi yake ya asili nayo ni mshambuliaji wa mwisho,tunapoteza kipaji cha huyu mtu kwa kumlazimisha acheze pembeni.Welbeck peke yake akichezeshwa kama striker wa mwisho ana uwezo wa kutupa magoli 20 kwenye msimu mmoja(hapo kumbuka tunawashambuliaji wengine 3)
4.CHICHARITO NI SUB. SIO MCHEZAJI WA KUANZA
Hili halihitaji kwenda shule kujua kuwa huyu mshambuliaji hawezi kulet sumu akianza.
Akitokea sub anafunga na kuibeba team,mchezo unaokuja Ferguson anampa nafasi ya kuanza anahangaika uwanjani bila kujielewa,unaokuja anawekwa benchi,anaingia na kufunga..je na hili linahitaji shule???
5.KAMA USIPOCHEZA VIZURI UKAE NJE.
Sisemi mchezaji akishindwa kuwa kwenye form kwenye mechi moja ndio awekwe benchi,hapana. Mchezaji akishindwa kupafom mechi kama mbili au tau sioni sababu ya yeye kuendelea kuanza,awe Rooney,RvP,De Gea,Carrick,Vidic..sioni sababu ya mchezaji kuchezshwa kwa mapenzi au jina kubwa au kisa kanunuliwa kwa bei mbaya.
Naamini tukifuata hizi njia 5 basi tutarudisha kombe letu Old Trafford,swali ni JE,UNAKUBALIANA NA HIZI NJIA 5????

Carrick,
Chicharito,
De Gea,
Rooney,
RvP
Man Utd kufaidika na ugomvi kati ya Inter Milan na Sneijder!
Mgongano wa kimaslahi unaoendelea sasa hivi kati ya Club ya Inter Milan na kiungo wao Wesley Sneijder unaweza ukawa na manufaa kwa Man Utd kutumia hii nafasi na kumnyakua kupitia dirisha dogo la usajili hapo January!
Wesley Sneijder analazimishwa kusaini mkataba mpya utakaopunguza mshahara wake wa sasa £200,000 kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayoikumba nchi ya Italia.
Matatizo hayo yamepelekea Inter kumuuza kipa wao Julio Cesar kwenda QPR.
Mkurugenzi wa Inter,Marco Branca amenukuliwa akisema '' kwa sasa tunaendelea kujadiliana naye,tunahitaji kumpa mkataba mpya na kupunguza mshahara,hatutamtumia kwenye mchezo wowote hadi akubali kusaini''

Inter Milan,
Julio Cesar,
Man Utd,
Marco Branca,
Wesley Sneijder
Anderson amejikatia ''tiketi'' ya kuanza dhidi ya West Ham Jumatano
Kiungo mchezeshaji mwenye uraia wa Brazil anayekipiga na Man Utd amefanikiwa kumshawishi Sir Alex Ferguson kuanza mechi ya Jumatano dhidi ya West Ham itakayopigwa nyumbani Old Trafford!
''Nadhani Anderson alibeba ushindi wetu Jumamosi,alicheza kwa kujiamni na kwa kujituma sana,hiyo imepelekea kujitengea nafasi ya kuanza Jumatano hii'' Ferguson alikiambia kituo cha Televisheni cha Manchester United.
Hivi karibuni Anderson amekua akipokea tuhuma kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka kuwa hawezi kuulinda mwili wake,watu mbalimbali wamekuwa wakisema ameongezeka sana na hivyo kuwa mzito.
Tuhuma hizi zimepelekea Anderson kushangilia goli la Chicharito(alilotoa pasi yeye) kwa kufunua jezi yake kama ishara ya kujibu tuhuma za wanaodai hayuko fiti kiafya.
Manchester United inacheza na West Ham kama muendelezo wa mechi za ligi kuu Jumatano hii Old Trafford saa tano usiku (23:00) kabla ya kusafiri Jumamosi kuifuata Reading,mechi itakayochezwa saa mbili na nusu usiku (20:30)

Sunday, November 11, 2012
THE COMEBACK KINGS>>Mara 8 Msimu Tukitoka Nyuma
Mara ya 8 hii msimu huu tunatokea nyuma na kushinda..natumaini beki zetu zote zikipona tutakuwa na
1.The best defensive options in Europe
2.The best striking force in Europe
Tuombe uzima
CHIGOALSITO>> JAVIER HERNANDEZ
Labels:
Javier Hernandez Chicharito
Friday, November 9, 2012
GARY NEVILLE AZUIWA KUONGEZA UREFU WA JENGO LAKE NJE YA OLD TRAFFORD
Man Utd wamewasilisha kwa maandishi pingamizi lao halmashauri la Garry Nevile kutaka kuongeza urefu wa Hotel yake anayotarajia kujenga ya ghorofa kumi,hoteli hiyo iko karibu na uwanja wa Old Trafford. Garry Nevile anataka kuongeza urefu ili AWEKE UWANJA WA MPIRA NA BAR KWA JUU YA HOTELI kitendo ambacho uongozi wa Man United umesema Hoteli itazuia muonekano wa upande wa mashariki mwa uwanja ambao ndo upande muhimu kwa mapato na utalii wa eneo hilo.
Labels:
Gary Neville,
Old Trafford
Thursday, November 8, 2012
Tuesday, November 6, 2012
QUOTES 10 BORA TOKA KWA SAF
1) After winning CL in 1999: “I can’t believe it. I can’t believe it. Football. Bloody hell.”
2) On Mourinho: “He was certainly full of it, calling me boss and big man when we had our post-match drink after the first leg. But it would help if his greetings were accompanied by a decent glass of wine. What he gave me was paint-stripper.”
3) On Wenger (2005): “In the tunnel, Wenger was criticising my players, calling them cheats, so I told him to leave them alone and behave himself. He ran at me with his hands raised saying 'What do you want to do about it?' To not apologise for the behaviour of the players to another manager is unthinkable. It's a disgrace, but I don't expect Wenger to ever apologise...he's that type of person.”
4) On winning record 19 PL titles: “My greatest challenge is not what’s happening at the moment, my greatest challenge was knocking Liverpool right off their f***ing perch. And you can print that.”
5) On Giggsy: “I remember the first time I saw him. He was 13 and just floated over the ground like a cocker spaniel chasing a piece of silver paper in the wind.”

Alex Ferguson,
Ryan Giggs
Thursday, October 11, 2012
ROONEY AFURAHIA KUCHAGULIWA KUWA CAPTAIN WA ENGLAND
“To be named as England captain for tomorrow's World Cup qualifier game is one of the proudest moments of my football career”
- Wayne Rooney ♥
Labels:
England,
Wayne Rooney
Sunday, October 7, 2012
ASHLEY YOUNG AKAA CHANGANYIKENI MECHI YA NEWCASTLE>>FAIRPLAY
Hii si mara yake ya kwanza, Ashley Young Hupenda kukaa sana na mashabiki, kusign autography baada ya mechi, Si rahisi kuona wachezaji wakifanya hivyo lakini, yeye hufanya hivyo. RESPECT FOR THIS
Katika Mechi Hiyo MANCHESTER UNITED ILISHINDA Bao 3 Kwa Bila, kwa magoli ya Vichwa ya Johny Evans na Patrice Evra, na lile la kushangaza la Tom Cleverley
Labels:
Ashley Young,
Johny Evans,
Patrice Evra,
Tom Cleverley
Saturday, October 6, 2012
DOGO ALIYEPIGA DEBE ROONEY ANUNULIWE
Huyo Dogo aliwahi kuingia Old Trafford na Bango lake na baada ya mechi kuisha alibaki uwanjani peke yake hadi akaja kutolewa na security.
Siku iliyofuata alienda uwanja wa mazoezi na Bango lake hadi kwa Sir Alex na kumwambia
"Rooney will help us please Buy him"
(Miss B)
Labels:
Alex Ferguson,
Wayne Rooney
Saturday, September 29, 2012
Baba Wa Ryann Tunniclife Ashinda Kamari
Ryan Tunnicliffe (ana miaka 19)...alipokuwa na miaka 9 yani miaka 10 iliyopita baba yake aliweka paundi 100 kucheza kamari kuwa ipo siku mwanae ataichezea Manchester United. Katika mchezo wa juzi wa Capital One cup kati ya Man Utd na Newcastle Utd, Tunnicliffe aliingia dakika ya 77 na kuweka historia ya kuichezea Man Utd mchezo wa kwanza wa kimashindano wa timu ya wakubwa na kumfanya baba yake ashinde paundi 10,000 (ni zaidi ya sh milioni 20 za Tz)...katika mchezo huo Man Utd iliifunga Newcastle Utd 2-1 na kufuzu kwa hatua inayofuata.
Labels:
Ryan Tunnicliffe
Saturday, September 22, 2012
RATING ZA WACHEZAJI WA MAN-UTD FIFA13
MANCHESTER UNITED FIFA 13 RATINGS :
Starting 11 (4-4-1-1):
GK. David De Gea, 80
RB. Rafael da Silva, 77
RCB. Nemanja Vidic, 89
LCB. Rio Ferdinand, 83
LB. Patrice Evra, 83
RM. Antonio Valencia, 83
RCM. Michael Carrick, 81
LCM. Paul Scholes, 81
LM. Ashley Young, 82
CF. Wayne Rooney, 89
ST. Robin van Persie, 88
Substitutes:
GK. Anders Lindegaard, 78
CB. Phil Jones, 78
CAM. Shinji Kagawa, 83
LM. Nani, 85
CAM. Thomas Cleverley, 78
ST. Javier Hernandez, 82
ST. Danny Welbeck, 79
Starting 11 (4-4-1-1):
GK. David De Gea, 80
RB. Rafael da Silva, 77
RCB. Nemanja Vidic, 89
LCB. Rio Ferdinand, 83
LB. Patrice Evra, 83
RM. Antonio Valencia, 83
RCM. Michael Carrick, 81
LCM. Paul Scholes, 81
LM. Ashley Young, 82
CF. Wayne Rooney, 89
ST. Robin van Persie, 88
Substitutes:
GK. Anders Lindegaard, 78
CB. Phil Jones, 78
CAM. Shinji Kagawa, 83
LM. Nani, 85
CAM. Thomas Cleverley, 78
ST. Javier Hernandez, 82
ST. Danny Welbeck, 79
Labels:
Fifa 13
Thursday, September 20, 2012
MABAO MATANO BORA YA RAUNDI YA NNE LIGI KUU YA UINGEREZA: BAO LA ALEX BUTTNER LAJUMUISHWA
1. Matthew Lowton (Aston Villa v Swansea)
Thursday, September 13, 2012
COMPLETE SET OF A PLAYER..AV7
Ashley Young is the latest Manchester United team-mate to express his admiration for Antonio Valencia, declaring his fellow winger "has it all".
Young, who hopes to be fit to face Valencia's former club Wigan Athletic on Saturday, was not surprised that the Ecuadorian was voted United’s double Player of the Year in 2011/12.
When asked by Inside United what made Valencia so effective, Young said: "Last season he had everything.
"He attacks, he defends, he can shoot, he can cross, he can pass... he has it all and that's why he scooped up everything at the end-of-season awards. It's why the players voted for him and it's why the fans voted for him.
"He's fantastic to play with. Antonio, like every other player, knows how to look after himself as well – he knows what to eat, what to drink and he works closely with our fitness coaches."
Valencia, who will face Wigan for the fifth time as a United player if he features this weekend, also earned plaudits from his manager.
"Antonio is always very professional and a great human being. I'm very happy with him," said Sir Alex this week.
"He’s one of those players who is constantly maturing. Without doubt, his best position is wide right – he’s fantastic there."
Tuesday, September 11, 2012
Mifumo 5 Man United Itakayoweza Kuitumia Msimu Huu
Kagawa,RvP,Rooney,Valencia,Nani,Vidic,Ferdinand..unawatumiaje hawa watu msimuu huu??
4-4-2
Kwa hali iliyoko sasa kila mtu anaamini kuwa Kagawa bado hajaanza kutumiwa ipasavyo kama ilivyokuwa na team yake Dortmund huko Ujerumani,na mfumo huu ndiyo utaharibu kabisa,japo ni mfumo utakaofanya ''wakali wanne'' wa Man United wote waanze na pia bila kusahau ni mfumo uliotumika kwa miaka kadhaa sasa kuiletea Manchester United ubingwa na mafanikio mbali mbali lakini iwe wazi kuwa kumchezesha Rooney na RvP mbele sio kitu atakachotaka au kuweza RvP,kwa miaka mingi RvP anapendelea na ni moto akicheza kama ''mshambuliaji mpweke'' mbele na pia hii itazidi kumzuia Kagawa kucheza nafasi ya kiungo mshambuliaji kwani itamvuta kati na kufanya asimame na Carrick au Scholes kwenye kukaba huku akiweka kichwani kuwa Rooney na RvP ndiyo watu wa kwanza kushambulia zikifuatia na winga mbili(kulia na kushoto) halafu ndiyo aje yeye wa mwisho
4-2-3-1
Hii inaonekana kama ina mafanikio lakini itamzuia Ferguson kuingiza wachezaji nyota wake wote,RvP atasimama mbele kama inavyotakiwa lakini itasababisha Rooney apiganie nafasi na RvP au Kagawa,tofauti na 4-3-3 ni kwamba hii inaondoa umuhimu wa Tom Cleverly kwa kuongeza kiungo mkabaji mmoja hapo katikati na ambayo kwa inavyoonekana anaweza kucheza Jones na Carrick
4-3-3
Hii imesaidia kwa mechi hizi za mwanzo msimu huu,mbinu hii inamuweka RvP mbele peke yake na hadi sasa tumeshuhudia RvP akifunga goli 4 katika mechi 3 kutokana na mbinu hii,sema sasa inamuweka Rooney pabaya,pamoja na kuwa Rooney anaweza kubadilika na kucheza popote lakini swali ni je atamtoa mtu gani kwenye nafasi yake ya asili?Uwezo wa kucheza nafasi ya Valencia anao lakini ukweli ni kuwa Valencia ni mmoja ya watu muhimu sana kwenye ile nafasi dunia ya leo,na je kwa Carrick?hapana pia..bado tunamuhitaji mtu kama Carrick pale katikati,hii itafanya Rooney aonje benchi mara moja moja akipokezana na Kagawa.
4-5-1 au 3-6-1
Hii tena inaleta nyota wote wa United pamoja,inaua beki mmoja kati ya wanne wa mwisho na kuzalisha kazi mara mbili kwa mawinga,kila nyota atacheza nafasi aliyoizoea pale mbele,RvP atabaki peke yake kama kawaida,Rooney atacheza na Kagawa pembeni yake na shimoni katikati Jones na Carrick watatawala.
Hii itafanya mawinga wawe na kazi mara mbili,za kushambulia na kukaba,kwa kusimamisha milingoti mitatu nyuma ina maanisha kuwa winga za kulia na kushoto zitahitajika pia kurudi nyuma na kucheza namba mbili na tatu,hii inatia hamu ya kuona wakicheza kwani kwenye makaratasi inaonyesha kama inazaliasha goli 3-4 kwa kila mechi
3-4-3
Hii inaonekana ni mahususi kwa ajili ya kusaidia ukuta wa kukaba wa Man United,Kagawa anarudi shimoni na winga zote mbili zitahitajika zicheze kama beki na winga,itawachosha sana ila itasaidia kukaba LAKINI itambulike kuwa Manchester United siyo Chelsea,hawatataka kucheza mchezo wa kukaba kila saa kwa hio hii inaweza kutumika mara moja moja kwenye mechi ngumu tu.

Subscribe to:
Posts (Atom)