Ads 468x60px

Monday, November 26, 2012

MAAMUZI MATANO (5) YA KIUFUNDI YATAKAYOTUSAIDIA KUBEBA KOMBE LA 20

ZIFAHAMU NJIA TANO ALIZOTOA MMOJA WA MASHABIKI WA MAN UTD KUELEKEA KOMBE LA 20.

Baada ya Chelsea na City kudroo mechi yao na sisi kurudi kileleni ,tena baada ya kupoteza michezo mitatu katika 13 tuliyocheza hadi sasa ni dhahiri kuwa taji la 20 sio shida kulibeba,endapo tutafanya mmamuzi haya matano ya kiufundi yatakayoweza kutusaidia kubeba ndoo ya 20.

1.GIGGS & SCHOLES WAAGE SASA NA KUONDOKA KWA AMANI.
Nawapenda sana hawa maveterani  wa soka na wameisaidia United katika kila namna hadi tumefikia hapa tulipo leo.
Baada ya kutizama mechi zetu mbili dhidi ya QPR na NORWICH na kuona jinsi hawa maveterani wanavyotaabika katikati na ukizingatia sio dhidi ya Barcelona au Madri basi utakubaliana na mimi kuwa wakati umeshawatupa mkono.Wnahitaji kustaafu kwa heshima,tuna wachezaji wengi na wazuri zaidi yao katika hilo eneo,ni muda sasa wawapishe damu changa wafanye kazi.


2. DAVID DE GEA ACHEZE KILA MCHEZO WA ''LIGI KUU''
Nafahamu kuwa alikuwa anaumwa na hakuweza kucheza dhidi ya Norwich lakini De Gea alitakiwa awepo golini katika mechi dhidi ya QPR,uwepo wake kabla ya Anderson kuja kunyanyua team ungetusaidia sana.De Gea anafanya kazi ambayo Lindegaard yeye kwake ni ndoto kuifanya,hawezi kufikia kiwango cha De Gea. De Gea ametuokoa sana na kutubeba msimu uliopita hadi kufikia kupoteza kombe kwa tofauti ya magoli.
Huu ni muda wa Ferguson kulazimisha huyu aanze kila mchezo wa ligi kuu.


3.ACHA KUMCHEZESHA WELBECK PEMBENI

Hili ni somo ambalo liko wazi sana kwa kila mtu kuona.England ni mwalimu wetu kwenye hili somo,Danny amekuwa kwenye form akicheza na team ya taifa kwa kuwa anachezeshwa katika nafasi yake ya asili nayo ni mshambuliaji wa mwisho,tunapoteza kipaji cha huyu mtu kwa kumlazimisha acheze pembeni.Welbeck peke yake akichezeshwa kama striker wa mwisho ana uwezo wa kutupa magoli 20 kwenye msimu mmoja(hapo kumbuka tunawashambuliaji wengine 3)


4.CHICHARITO NI SUB. SIO MCHEZAJI WA KUANZA
Hili halihitaji kwenda shule kujua kuwa huyu mshambuliaji hawezi kulet sumu akianza.
Akitokea sub anafunga na kuibeba team,mchezo unaokuja Ferguson anampa nafasi ya kuanza anahangaika uwanjani bila kujielewa,unaokuja anawekwa benchi,anaingia na kufunga..je na hili linahitaji shule???


5.KAMA USIPOCHEZA VIZURI UKAE NJE.
Sisemi mchezaji akishindwa kuwa kwenye form kwenye mechi moja ndio awekwe benchi,hapana. Mchezaji akishindwa kupafom mechi kama mbili au tau sioni sababu ya yeye kuendelea kuanza,awe Rooney,RvP,De Gea,Carrick,Vidic..sioni sababu ya mchezaji kuchezshwa kwa mapenzi au jina kubwa au kisa kanunuliwa kwa bei mbaya.

Naamini tukifuata hizi njia 5 basi tutarudisha kombe letu Old Trafford,swali ni JE,UNAKUBALIANA NA HIZI NJIA 5????

0 comments:

Post a Comment