Ads 468x60px

Tuesday, November 27, 2012

ASHLEY YOUNG,UVUMILIVU UNATUSHINDA!

Wakati Boss anaenda kumwaga £17M kumnunua Young watu wengi walishtuka kidogo,tulikuwa bado tuna uwezo wa kuwachezesha Rooney,Welbeck na Luis Nani upande ule wa kushoto(kama tatizo lilikuwa ni mtu wa kucheza kushoto) Kuongezea hilo bado tulikuwa na Fabio na Giggs ambao wangeweza kuokoa hiyo pesa iliyoenda kwa Young!! Hatusemi tumenunua plastiki,la hasha ila maisha ya uwezo wa Young yalidumu kwa muda wa miezi mitatu tu ya mwanzo,baada ya hapo kama sio majeraha basi itakuwa ni kucheza chini ya kiwango,matatizo baada ya matatizo!


Nadiriki kusema timu ya ''scouting'' ilifanya mahesabu mabaya,ni muda huo huo mashabiki tulikua tunatarajia babu atanunua wachezaji 2 au 1 kwenye nafasi ya kiungo mkabaji,lakini matarajio yetu yakawa ndivyo sivyo,akaja kijana mwingine kujaza kontena la mawinga tulionao.
Sisemi Young ni mchezaji mbaya kiasi cha kufikia hatua ya kumfananisha na Bebe,hapana. Msimu wake wa kwanza United alitupa magoli 6 na Assists 9,sio mbaya kwa winga..lakini ni mbaya kwa winga wa £17M aliyerekodi assists 17 msimu wake wa kwanza Aston Villa na Assists 14 msimu wa mwisho kabla hajasajiliwa Man United.
Kwa hali ilivyo sasa, majeruhi Nani na Kagawa wakipona tutaanza kusahau uwepo wa Young,hasa pale babu akiamua kutumia mfumo wa ''diamond'' 4-3-3 uliotuletea mafanikio makubwa dhidi ya Braga na New Castle msimu huu.
Valencia anaweza kuwa kwenye form mbovu msimu huu lakini bado ana uwezo wa kulaza mabeki wawili au watatu na kulazimisha krosi ndani.

NI WAKATI WA YOUNG KUTHIBITISHA KUWA HATUKUFANYA MAKOSA KUONGEZA WINGA WAKATI TUNA MATATIZO YA KIUNGO MKABAJI,HILI LINAWEZA LIKAWA MZIGO NA MTIHANI KWAKE LAKINI MWISHO WA SIKU ANALIPWA ILI AFANYE HII KAZI.

0 comments:

Post a Comment