Ads 468x60px

Monday, November 26, 2012

Man Utd kufaidika na ugomvi kati ya Inter Milan na Sneijder!

Mgongano wa kimaslahi unaoendelea sasa hivi kati ya Club ya Inter Milan na kiungo wao Wesley Sneijder unaweza ukawa na manufaa kwa Man Utd kutumia hii nafasi na kumnyakua kupitia dirisha dogo la usajili hapo January!

Wesley Sneijder analazimishwa kusaini mkataba mpya utakaopunguza mshahara wake wa sasa £200,000 kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayoikumba nchi ya Italia.
Matatizo hayo yamepelekea Inter kumuuza kipa wao Julio Cesar kwenda QPR.

Mkurugenzi wa Inter,Marco Branca amenukuliwa akisema '' kwa sasa tunaendelea kujadiliana naye,tunahitaji kumpa mkataba mpya na kupunguza mshahara,hatutamtumia kwenye mchezo wowote hadi akubali kusaini''


0 comments:

Post a Comment