Swansea wamekuwa ni nyoka wenye sumu kali sana hasa wanavyokutana na timu kubwa,wanaongeza umakini kwenye mechi na hayo yoyte yanatetea na mtu mmoja tu,mshambuliaji wao hataaaari asiye na huruma na nyavu MICHU!
Upande wa pili wa shilingi unaowazungumzia wageni ambao ni vinara wa ligi kwa tofauti ya point 6,Man United una sumu kali mara mbili ya hawa wanaoitwa Swanselona.ujio wa Robin Van Persie kutoka Arsenal umeongeza sumu ya United huku akisaidiwa na striker mwenzake mwenye uwezo wa kucheza namba yoyote uwanjani(hata golikipa) Wayne ''Wazzaaa'' Rooney.
Rooney na Van Persie msimu huu wameanza pamoja mara 12 na mechi zote hizo United kashinda zote. Inasadikika pacha yao ndo pacha hatari kwa sasa ligi kuu ukizingatia Robin Van Persie yuko pale juu akiminyana na Michu kwa idadi ya magoli kumi na mbili kila mmoja.
VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA KWENYE HII MECHI
*Mara ya mwisho Swansea wanashinda mechi ya nyumbani dhidi ya Man United ilikuwa Januari 1982
*Swansea wamefunga goli moja tu kutoka kwenye mipira iliyokufa msimu huu,mengine yote yaliyobaki 25 wamefunga kwenye mchezo wa pasi
*Hadi sasa Man United magoli yake yamefungwa na wachezaji 15 tofauti
*Man United wanaongoza kwa magoli ya krosi (14) msimu huu na pia wanaongoza kwa magoli ya vichwa(10) msimu huu
WACHEZAJI WA KUWAANGALIA
SWANSEA.
MICHU
Umakini wake na njaa yake ya magoli haufanani na pesa kidogo aliyonunuliwa £2m
Ni hatari sana hasa kama United wataendelea na mchezo wa mabeki wake kujisahau
Ana magoli 12 katika game 17 alizoanza,huku akifunga 6 katika michezo yake 6 ya mwisho
MAN UTD
ROBIN VAN PERSIE
Kwa baadhi ya amshabiki wa United ni kama bado wako kwenye ndoto,hawaamini kama huyu muuaji amekubali kutua Old Trafford kutokea Arsenal,ameisaidia sana na kuitoa Man United shimoni msimu huu
Ni kinara wa magoli pamoja na Michu wote wakiwa na magoli 12 pale juu
MAJERUHI
Man United bado itaendelea kuwakosa Luis Nani,RafaelAnderson,Kagawa huku Vidic akipatikana lakini kuwa na uwezekano mdogo wa kuanza hii mechi. Evans na yeye amepona na kwa taarifa kutoka kwa kocha ni kuwa anaweza kucheza.
0 comments:
Post a Comment