Ads 468x60px

Monday, November 26, 2012

Anderson amejikatia ''tiketi'' ya kuanza dhidi ya West Ham Jumatano

Kiungo mchezeshaji mwenye uraia wa Brazil anayekipiga na Man Utd amefanikiwa kumshawishi Sir Alex Ferguson kuanza mechi ya Jumatano dhidi ya West Ham itakayopigwa nyumbani Old Trafford!

''Nadhani Anderson alibeba ushindi wetu Jumamosi,alicheza kwa kujiamni na kwa kujituma sana,hiyo imepelekea kujitengea nafasi ya kuanza Jumatano hii'' Ferguson alikiambia kituo cha Televisheni cha Manchester United.

Hivi karibuni Anderson amekua akipokea tuhuma kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka kuwa hawezi kuulinda mwili wake,watu mbalimbali wamekuwa wakisema ameongezeka sana na hivyo kuwa mzito.
Tuhuma hizi zimepelekea Anderson kushangilia goli la Chicharito(alilotoa pasi yeye) kwa kufunua jezi yake kama ishara ya kujibu tuhuma za wanaodai hayuko fiti kiafya.


Manchester United inacheza na West Ham kama muendelezo wa mechi za ligi kuu Jumatano hii Old Trafford saa tano usiku (23:00) kabla ya kusafiri Jumamosi kuifuata Reading,mechi itakayochezwa saa mbili na nusu usiku (20:30)


0 comments:

Post a Comment