Ads 468x60px

Wednesday, November 28, 2012

KUELEKEA MCHEZO WA LEO USIKU DHIDI YA WEST HAM

Man United usiku wa leo inawakaribisha vijana waliopanda daraja msimu huu WEST HAM UNITED wanaoshikilia nafasi ya 8 kwenye ligi hadi sasa.



MANCHESTER UNITED
Michezo 5 ya mwisho W W L W W
Mchezo wa mwisho Man Utd 3-1 QPR

WEST HAM UNITED
Michezo 5 ya mwisho L D W D L
Mchezo wa mwisho Tottenham 3- 1 West Ham

Kagawa anaweza kucheza baada ya kufanikiwa kupona,Nani na Vidic bado ni majeruhi pamoja na Valencia. Kama alivyosema Ferguson,Anderson ataanza mchezo na West Ham baada ya kucheza vizuri mechi iliyopita dhidi ya QPR.
Matatizo yanayoikumba Man Utd ya mabeki yanaweza kuwa yameisha baada ya uhakika wa kuwepo kwa Rio Ferdinand,Evans,Smallin na Jones huku Scholes akiwa kwenye adhabu baada ya kupokea kadi yake ya 5 ya njano dhidi ya QPR mechi iliyopita.

HATIMAYE KITABU CHA MAISHA YA WACHEZAJI WA MAN UTD ''SONS OF UNITED'' CHAKAMILIKA

Hatimaye kile kitabu kilichotumia miaka 18,kilichoandikwa na mfanyabiashara wa Droitwich Spa kimekamilika..
Kitabu hicho kinachoelezea kwa kina maisha ya makinda wa Man Utd kuanzia wakiwa wadogo na mahojiano pamoja na picha kiko sokoni,Steve Hobin amefanya mahojiano na wachezaji wengi kwenye kitabu hicho kuanzia Bobby Charlton,Ryan Giggs,Beckham na Scholes kimeshaanza kununuliwa kupitia internet ulimwenguni kote.

Kitabu hicho kina kurasa 576 na kimechapisha nakala 2,000 tu!

Tuesday, November 27, 2012

TAARABT KUTUA OLD TRAFFORD????

Kiungo mchezeshaji wa Morroco Adel Taarabt anaweza kutua Old Trafford January hii,hii inatokana na kuwasili kwa kocha mpya QPR Harry Redknapp,hapo mwanzo wakati anatoka Lens na kutua Tottenham
 alibeba matumaini ya watu wengi huku wengine wakidiriki kumuita ''Zidane Mpya'',hakuwa na mahusiano mazuri na Harry Redknapp hadi kupelekea kuuzwa QPR na kocha huyo,sasa kocha huyo kamwaga wino QPR kuna uwezekano wa kiungo huyo kutua Old Trafford kwani amekuwa kwenye akili ya Babu kwa muda sasa.

CLEVERLEY KUFUNGWA PINGU OLD TRAFFORD

Baadhi ya wachambuzi wa soka wameshaanza kumvisha majukumu mazito kwa kumfananisha na Paul Scholes,kiungo huyu kinda wa Man Utd anatarajia kupewa mkataba wa muda mrefu ifikapo mwaka mpya.
Kwa sasa Cleverley mkataba wake ni £35,000 hivyo anatarajia kutia saini mkataba wa miaka mitano utakaofanya alipwe sasa £60,000 kwa wiki!


Kiwango chake kwa sasa hakijamuwezesha kukaa chini na kujadili mkataba mpya,bali hata kupata namba ya uhakika kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza!

Babu anatarajia kuwapa mikataba ya kifungo kirefu wachezaji wake wote wadogo kama njia ya kutengeneza misingi ya baadae ya klabu,wengine walioko kwenye hatua hiyo ni Smalling,Jones na Chicharito.

ASHLEY YOUNG,UVUMILIVU UNATUSHINDA!

Wakati Boss anaenda kumwaga £17M kumnunua Young watu wengi walishtuka kidogo,tulikuwa bado tuna uwezo wa kuwachezesha Rooney,Welbeck na Luis Nani upande ule wa kushoto(kama tatizo lilikuwa ni mtu wa kucheza kushoto) Kuongezea hilo bado tulikuwa na Fabio na Giggs ambao wangeweza kuokoa hiyo pesa iliyoenda kwa Young!! Hatusemi tumenunua plastiki,la hasha ila maisha ya uwezo wa Young yalidumu kwa muda wa miezi mitatu tu ya mwanzo,baada ya hapo kama sio majeraha basi itakuwa ni kucheza chini ya kiwango,matatizo baada ya matatizo!


Nadiriki kusema timu ya ''scouting'' ilifanya mahesabu mabaya,ni muda huo huo mashabiki tulikua tunatarajia babu atanunua wachezaji 2 au 1 kwenye nafasi ya kiungo mkabaji,lakini matarajio yetu yakawa ndivyo sivyo,akaja kijana mwingine kujaza kontena la mawinga tulionao.
Sisemi Young ni mchezaji mbaya kiasi cha kufikia hatua ya kumfananisha na Bebe,hapana. Msimu wake wa kwanza United alitupa magoli 6 na Assists 9,sio mbaya kwa winga..lakini ni mbaya kwa winga wa £17M aliyerekodi assists 17 msimu wake wa kwanza Aston Villa na Assists 14 msimu wa mwisho kabla hajasajiliwa Man United.
Kwa hali ilivyo sasa, majeruhi Nani na Kagawa wakipona tutaanza kusahau uwepo wa Young,hasa pale babu akiamua kutumia mfumo wa ''diamond'' 4-3-3 uliotuletea mafanikio makubwa dhidi ya Braga na New Castle msimu huu.
Valencia anaweza kuwa kwenye form mbovu msimu huu lakini bado ana uwezo wa kulaza mabeki wawili au watatu na kulazimisha krosi ndani.

NI WAKATI WA YOUNG KUTHIBITISHA KUWA HATUKUFANYA MAKOSA KUONGEZA WINGA WAKATI TUNA MATATIZO YA KIUNGO MKABAJI,HILI LINAWEZA LIKAWA MZIGO NA MTIHANI KWAKE LAKINI MWISHO WA SIKU ANALIPWA ILI AFANYE HII KAZI.

Monday, November 26, 2012

MAAMUZI MATANO (5) YA KIUFUNDI YATAKAYOTUSAIDIA KUBEBA KOMBE LA 20

ZIFAHAMU NJIA TANO ALIZOTOA MMOJA WA MASHABIKI WA MAN UTD KUELEKEA KOMBE LA 20.

Baada ya Chelsea na City kudroo mechi yao na sisi kurudi kileleni ,tena baada ya kupoteza michezo mitatu katika 13 tuliyocheza hadi sasa ni dhahiri kuwa taji la 20 sio shida kulibeba,endapo tutafanya mmamuzi haya matano ya kiufundi yatakayoweza kutusaidia kubeba ndoo ya 20.

1.GIGGS & SCHOLES WAAGE SASA NA KUONDOKA KWA AMANI.
Nawapenda sana hawa maveterani  wa soka na wameisaidia United katika kila namna hadi tumefikia hapa tulipo leo.
Baada ya kutizama mechi zetu mbili dhidi ya QPR na NORWICH na kuona jinsi hawa maveterani wanavyotaabika katikati na ukizingatia sio dhidi ya Barcelona au Madri basi utakubaliana na mimi kuwa wakati umeshawatupa mkono.Wnahitaji kustaafu kwa heshima,tuna wachezaji wengi na wazuri zaidi yao katika hilo eneo,ni muda sasa wawapishe damu changa wafanye kazi.


2. DAVID DE GEA ACHEZE KILA MCHEZO WA ''LIGI KUU''
Nafahamu kuwa alikuwa anaumwa na hakuweza kucheza dhidi ya Norwich lakini De Gea alitakiwa awepo golini katika mechi dhidi ya QPR,uwepo wake kabla ya Anderson kuja kunyanyua team ungetusaidia sana.De Gea anafanya kazi ambayo Lindegaard yeye kwake ni ndoto kuifanya,hawezi kufikia kiwango cha De Gea. De Gea ametuokoa sana na kutubeba msimu uliopita hadi kufikia kupoteza kombe kwa tofauti ya magoli.
Huu ni muda wa Ferguson kulazimisha huyu aanze kila mchezo wa ligi kuu.


3.ACHA KUMCHEZESHA WELBECK PEMBENI

Hili ni somo ambalo liko wazi sana kwa kila mtu kuona.England ni mwalimu wetu kwenye hili somo,Danny amekuwa kwenye form akicheza na team ya taifa kwa kuwa anachezeshwa katika nafasi yake ya asili nayo ni mshambuliaji wa mwisho,tunapoteza kipaji cha huyu mtu kwa kumlazimisha acheze pembeni.Welbeck peke yake akichezeshwa kama striker wa mwisho ana uwezo wa kutupa magoli 20 kwenye msimu mmoja(hapo kumbuka tunawashambuliaji wengine 3)


4.CHICHARITO NI SUB. SIO MCHEZAJI WA KUANZA
Hili halihitaji kwenda shule kujua kuwa huyu mshambuliaji hawezi kulet sumu akianza.
Akitokea sub anafunga na kuibeba team,mchezo unaokuja Ferguson anampa nafasi ya kuanza anahangaika uwanjani bila kujielewa,unaokuja anawekwa benchi,anaingia na kufunga..je na hili linahitaji shule???


5.KAMA USIPOCHEZA VIZURI UKAE NJE.
Sisemi mchezaji akishindwa kuwa kwenye form kwenye mechi moja ndio awekwe benchi,hapana. Mchezaji akishindwa kupafom mechi kama mbili au tau sioni sababu ya yeye kuendelea kuanza,awe Rooney,RvP,De Gea,Carrick,Vidic..sioni sababu ya mchezaji kuchezshwa kwa mapenzi au jina kubwa au kisa kanunuliwa kwa bei mbaya.

Naamini tukifuata hizi njia 5 basi tutarudisha kombe letu Old Trafford,swali ni JE,UNAKUBALIANA NA HIZI NJIA 5????

Man Utd kufaidika na ugomvi kati ya Inter Milan na Sneijder!

Mgongano wa kimaslahi unaoendelea sasa hivi kati ya Club ya Inter Milan na kiungo wao Wesley Sneijder unaweza ukawa na manufaa kwa Man Utd kutumia hii nafasi na kumnyakua kupitia dirisha dogo la usajili hapo January!

Wesley Sneijder analazimishwa kusaini mkataba mpya utakaopunguza mshahara wake wa sasa £200,000 kutokana na matatizo ya kiuchumi yanayoikumba nchi ya Italia.
Matatizo hayo yamepelekea Inter kumuuza kipa wao Julio Cesar kwenda QPR.

Mkurugenzi wa Inter,Marco Branca amenukuliwa akisema '' kwa sasa tunaendelea kujadiliana naye,tunahitaji kumpa mkataba mpya na kupunguza mshahara,hatutamtumia kwenye mchezo wowote hadi akubali kusaini''


Anderson amejikatia ''tiketi'' ya kuanza dhidi ya West Ham Jumatano

Kiungo mchezeshaji mwenye uraia wa Brazil anayekipiga na Man Utd amefanikiwa kumshawishi Sir Alex Ferguson kuanza mechi ya Jumatano dhidi ya West Ham itakayopigwa nyumbani Old Trafford!

''Nadhani Anderson alibeba ushindi wetu Jumamosi,alicheza kwa kujiamni na kwa kujituma sana,hiyo imepelekea kujitengea nafasi ya kuanza Jumatano hii'' Ferguson alikiambia kituo cha Televisheni cha Manchester United.

Hivi karibuni Anderson amekua akipokea tuhuma kutoka kwa mashabiki na wachambuzi wa soka kuwa hawezi kuulinda mwili wake,watu mbalimbali wamekuwa wakisema ameongezeka sana na hivyo kuwa mzito.
Tuhuma hizi zimepelekea Anderson kushangilia goli la Chicharito(alilotoa pasi yeye) kwa kufunua jezi yake kama ishara ya kujibu tuhuma za wanaodai hayuko fiti kiafya.


Manchester United inacheza na West Ham kama muendelezo wa mechi za ligi kuu Jumatano hii Old Trafford saa tano usiku (23:00) kabla ya kusafiri Jumamosi kuifuata Reading,mechi itakayochezwa saa mbili na nusu usiku (20:30)


Sunday, November 11, 2012

THE COMEBACK KINGS>>Mara 8 Msimu Tukitoka Nyuma

 
Mara ya 8 hii msimu huu tunatokea nyuma na kushinda..natumaini beki zetu zote zikipona tutakuwa na
1.The best defensive options in Europe
2.The best striking force in Europe

Tuombe uzima

CHIGOALSITO>> JAVIER HERNANDEZ

Photo: Unafuraha kiasi gani kuhusu mechi ya jana!
Embu sema neno kuhusu huyu kijana Hernandez

¤Shebby¤

Friday, November 9, 2012

GARY NEVILLE AZUIWA KUONGEZA UREFU WA JENGO LAKE NJE YA OLD TRAFFORD

 
Man Utd wamewasilisha kwa maandishi pingamizi lao halmashauri la Garry Nevile kutaka kuongeza urefu wa Hotel yake anayotarajia kujenga ya ghorofa kumi,hoteli hiyo iko karibu na uwanja wa Old Trafford. Garry Nevile anataka kuongeza urefu ili AWEKE UWANJA WA MPIRA NA BAR KWA JUU YA HOTELI kitendo ambacho uongozi wa Man United umesema Hoteli itazuia muonekano wa upande wa mashariki mwa uwanja ambao ndo upande muhimu kwa mapato na utalii wa eneo hilo.

Tuesday, November 6, 2012

QUOTES 10 BORA TOKA KWA SAF

http://img.skysports.com/11/11/640/Godfather-Sir-Alex-Ferguson-Opinion-25-Years_2674281.jpg 1) After winning CL in 1999: “I can’t believe it. I can’t believe it. Football. Bloody hell.”

2) On Mourinho: “He was certainly full of it, calling me boss and big man when we had our post-match drink after the first leg. But it would help if his greetings were accompanied by a decent glass of wine. What he gave me was paint-stripper.”


3) On Wenger (2005): “In the tunnel, Wenger was criticising my players, calling them cheats, so I told him to leave them alone and behave himself. He ran at me with his hands raised saying 'What do you want to do about it?' To not apologise for the behaviour of the players to another manager is unthinkable. It's a disgrace, but I don't expect Wenger to ever apologise...he's that type of person.”

4) On winning record 19 PL titles: “My greatest challenge is not what’s happening at the moment, my greatest challenge was knocking Liverpool right off their f***ing perch. And you can print that.”

5) On Giggsy: “I remember the first time I saw him. He was 13 and just floated over the ground like a cocker spaniel chasing a piece of silver paper in the wind.”