HABARI ZILIZOTHIBITISHWA NA
MTANDAO RASMI WA MANCHESTER
UNITED NI KWAMBA MCHEZAJI NICK
POWELL AMEJIUNGA NA KLABU YA
WIGAN ATHLETICS KWA MKOPO WA
MWAKA MMOJA NA BEBE AMEUZWA
KWA MKOPO KWA KLABU YA FC
PACOS DE FEREIRA YA URENO.
Monday, September 2, 2013
FELLAINI AKAMILISHA USAJILI KUJIUNGA NA MANCHESTER UNITED
KATIKA DAKIKA ZA MWISHO ZA DIRISHA LA USAJILI MANCHESTER UNITED IMEKAMILISHA USAJILI WA MCHEZAJI MOURAINE FELLAINI ALIYESAJILIWA KUTOKA KLABU YA EVERTON.
KWA KUJIUNGA NA UNITED FELLAINI ANAKUWA AMEUNGANA NA KOCHA WAKE WA ZAMANI DAVID MOYES WALIYEKUWA WOTE KLABU YA EVERTON
WELL DONE!! WELL DONE!!
VIVA MOYES
Thursday, August 29, 2013
NEWS ALERT: ANGELO HENRIQUEZ AJIUNGA NA REAL ZARAGOZA KWA MKOPO WA MWAKA MMOJA
Manchester United wamekubaliana na timu Real Zaragoza inayoshiriki Ligi Kuu ya Hispania maarufu kama La Liga kumsajili kwa mkopo wa mwaka mmoja mchezaji kinda wa Manchester United ambaye pia ni Raia wa Chile Angelo Henriquez.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 19 ataitumikia Real Zaragoza mpaka mwezi Juni Tarehe 30 Mwaka 2014.
Ikumbukwe pia mwaka jana Henriquez aliitumikia Wigan Athletic pia kwa mkopo.
KILA LA KHERI HENRIQUEZ
Monday, April 29, 2013
PFA TEAM OF THE YEAR: Rio, Carrick, De Gea & Van Persie Wajumuishwa
Newly-crowned champions Manchester United were well represented in the PFA’s team of the year for the Barclays Premier League – but there was no place for Wayne Rooney.
The selection by his fellow professionals of United number one David De Gea came as something of a surprise, especially given the quality of rival keepers in the top flight.Established figures such as Joe Hart, Petr Cech and Pepe Reina have come under siege from the likes of Simon Mignolet, Hugo Lloris and Asmir Begovic.
But the PFA vote went to De Gea who, after what can best be described as a ‘difficult’ start to his United career, has proved the doubters wrong and shown his true colours.
Many felt his slight frame would not stand up to the rigours of the English game, but he has shown in recent months he can mix it with the biggest. As we discovered when he was smashed by Andy Carroll recently, but dusted himself down and got on with the job.
Sky pundit Gary Neville suggested at the weekend that Rio Ferdinand was having one of his most consistent-ever seasons, even though he’s started just 25 games in the Premier and made only three Champions League appearances before United’s untimely exit.
Labels:
David De Gea,
Michael Carrick,
Rio Ferdinand,
Robin Van Persie
Wednesday, April 3, 2013
MANCHESTER UNITED ITAMSAJIRI JAMES RODRIGUEZ???
Upo uwezekano kwa klabu ya Manchester United kurudia nia yake ya
kutaka kumsajili winga machachari, kipaji halisi cha soka kutoka nchini
Colombia anakipiga FC Porto ya Ureno James Rodriguez. Inavyoonekana Man
United inaweza ikafanikiwa kupata huduma ya mchezaji huyu endapo tu
itakubali kubadilishana moja ya wachezaji wao ghali...anaweza akawa
Anderson au Antonio Valencia.
Rodriguez mwenye miaka 21 tu hivi sasa, amekuwa kwenye mawindo ya Sir Alex Ferguson kwa mda mrefu sasa tangu kipindi cha dirisha kubwa la usajili barani Ulaya katikati ya mwaka uliopita wa 2012. Man United ilipeleka ofa FC Porto lakini kwa bahati mbaya ilikataliwa. FC Porto walihitaji £36m, pesa ambayo ilikuwa ngumu kidogo United kukubali kuitoa.
Hata hivyo, kumekuwa na taarifa kutoka vyanzo mbalimbali nchini Uingereza kuwa kiungo Anderson angependa kurudi kwenye klabu yake ya zamani (FC Porto) kitu ambacho binafsi ninahisi kitasaidia kufanikisha lengo la United kumnasa Rodriguez.
Anderson amejikuta akiwa kwenye wakati mgumu ndani ya Manchester United kutokana na kushindwa kurudia fomu yake tangu apatwe na tatizo la kuandamwa na majeruhi na amekuwa akikabiliwa na upinzani wa hali ya juu kupata nafasi kwenye kikosi cha kwanza kutoka kwa kina Michael Carrick na kinda Tom Cleverley jambo ambalo linachochea hamu yake ya kutafuta timu nyingine atakayoichezea michezo mingi ili mwisho wa siku aitwe kwenye kikosi cha timu yake ya taifa ya Brazil kitakachocheza fainali za kombe la Dunia mwakani.
Pia kwa mujibu wa taarifa mbalimbali, ni wazi kwamba Manchester United inataka kuondokana na mchezaji huyo ambae kimsingi mtu anaweza kumuita 'injury prone player' yani mchezaji anaesumbuliwa na majeruhi ya mara kwa mara. United inataka kumrejesha Anderson FC Porto ili kuwe na urahisi fulani wa kumpata Rodriguez.
Na jambo lingine la kufurahisha ni kwamba msaka vipaji wa Man Utd Martin Ferguson ameki-scout kipaji hiki mara 7 msimu huu. Inaonekana sasa ni wazi kwamba Sir Alex Ferguson atawapa FC Porto Anderson na atatuma ofa mpya ya kutaka kumnasa Rodriguez.
James Rodriguez ameanza michezo 11 msimu huu na amefunga mabao 8 kwenye ligi kuu ya Ureno, na kama atajiunga na wababe hao wa soka la Uingereza itamaanisha atakuwa amejiunga na washambuliaji wa kiwango cha Dunia (World Class Players) Wayne Rooney na Robin van Persie kwenye safu ya ushambuliaji ya Manchester United...Rodriguez anasemwa kuwa bidhaa muhimu sana ambayo soka la Ulaya na Dunia kwa ujumla inajivunia nae.
Safari hii, mawinga wa United hawajaonesha makali sana tofauti na misimu kadhaa iliyopita. Baadhi yao wameporomoka viwango hasa Antonio Valencia ambae msimu uliopita ndie alikuwa mchezaji bora wa mwaka wa Manchester United...Ikiwa tayari Man United wameshamnasa Wilfried Zaha katika dirisha dogo la usajili lililopita la mwezi januari, ni wakati sasa wa United kuanza kutumia damu mpya kwenye 'flanks' ili kurejesha zile 'glorious days' kama za enzi ya Cristiano Ronaldo.
Zaidi ya hayo, James Rodriguez amekuwa akitajwa kama ndie Cristiano Ronaldo wa Amerika ya kusini kutokana na uwezo wake mkubwa alionao wa kusakata kabumbu. Pia mwenyewe alifarijika sana pindi aliposikia taarifa za kutakiwa na Manchester United msimu uliopita na baadae kunukuliwa akisema siku moja angependa kuchezea moja ya vilabu vikubwa barani Ulaya na akazitaja timu za Manchester United, Real Madrid na FC Barcelona.
Kwa kumalizia, kama Man United itafanikiwa kumsajili Rodriguez basi bila shaka itakuwa na safu moja kali sana ya ushambuliaji na haitakuwa ikipigania Ubingwa wa EPL pekee bali pia Ubingwa wa FA na Ubingwa wa Ulaya yani ile UEFA Champions League...TUSUBIRI TUONE!

Thursday, January 24, 2013
Giggs,The New United Coach???
Naomba nishirikiane na nyie kwenye hili,ni mawazo yangu binafsi najaribu kuchanganya picha ili nipate moja kubwa,nzuri na yenye muonekano halisi! Unayo ruhusa ya kuchangia kwa kupinga au kuongezea kitu..
KWANINI FERGUSON BADO ANA KAMA 3 OR 2 YEARS ZA KUFUNDISHA PALE OLD TRAFFORD NA NANI NAHISI ATAMRITHI.
1.Pep Guardiola
Hii ni sababu ya kwanza inayonipa kiburi cha kusema Ferguson bado tunaye,mwanzoni nilijiaminisha kama wenzangu kuwa huyu ndo mtu anayesubiri kupokea mikoba ya babu pale hasa ukizingatia style yake ya kufundisha inayothamini wachezaji wazawa na mchanganyiko kidogo wa ugenini ukiweka na kuwa ni mtu aliye na utayari wa kukaa kwenye club moja kwa muda mrefu kidogo kulinganisha na wengine! Baada ya kutangazwa rasmi kuwa anatua Bayern Munich sasa naamini SAF bado yuko pale Old Trafford.
2.David Moyes
Huyu ni kocha wa Everton ambaye wachambuzi mbali mbali wamekuwa wakimfananisha na Ferguson kwa kusema kuwa ana system ya uongozi nzuri kama ya babu kuanzia staff wa kawaida hadi uwanjani,wote wanakuwa wanamuangalia kama nyota ya team,ana uwezo binafsi wa kucontroll wachezaji nyota wasilete matatizo kwenye club na pia ni raia wa Scotland anapotoka SAF.
Hivi juzi kumekuwa na taarifa zinazosema kuwa huenda Chelsea wakamchukua yeye baada ya kumaliza list ya makocha wakubwa na ukizingatia matatizo ya mastaa pale Stamford wanaamini huyu ndo mwarobaini wao.Hili bado linazidi kunipa moyo kuwa bado tunaye babu sana.
3.Mourinho
Huyu tangu mwanzo namkubali kwa uwezo wake lakini tabia yake ya kubeba kobe na kukimbia haitamruhusu afunguliwe milango ya ukocha pale Old Trafford,United sio team ya kuhangaika kutafuta makocha kila mwisho wa msimu au miwili. Huyu nilijua na bado nahisi hatoweza kupewa ruhusa ya kuja pale.Sababu nyingine ya kwanini babu anaendelea kuwa kocha pale.
4.Usajili wa Wilfried Zaha
Endapo ndani ya masaa machache yajayo atatangazwa huyu kijana kutua Old Trafford basi inaniaminisha kuwa Babu kamchukua na ameamua kumuhangaikia kwa kuwa ana mpango naye,na kama ana mpango naye kwanini aondoke mwisho wa msimu? Babu bado tunaye pale Old Trafford kwa hii issue ya Zaha
5.Ryan Giggs na badge za ukocha
Hivi karibuni imefahamika kuwa Giggs atakuwa mchezaji wa kwanza kupewa ''leseni za awali'' za kufundisha huku akiwa mchezaji bado,hii inaniambia kuwa huyu kijana anapikwa chini kwa chini na Babu na hilo linatupeleka hadi misimu miwili au mitatu ijayo ambayo Babu atahakikisha amemuacha Giggs na kila kitu cha kuweza kutuongoza pale Old Trafford
CONCLUSION:
Nikijaribu kuunganisha picha zote hizo nagundua kuwa babu bado tunaye sana na kitu kinachombakiza ni kuhakikisha anamuacha Giggs katika kiti salama cha ukocha,baada ya kusema hivyo naomba niseme kuwa Giggs ndo kocha anyemrithi babu pale Old Trafford,hili litawashangaza sana watu!!! Ila ndo picha inapoelekea. Ukizingatia Giggs ni mchezaji aliyekaa pale toka '92 anayeijua timu vizuri na jinsi inavyoendeshwa.
Unaweza Kuongeza Au Kupinga Kwa Hoja..Karibu.
Labels:
Alex Ferguson,
Mourinho,
Moyes,
Pep Guardiola,
Ryan Giggs,
Zaha
Subscribe to:
Posts (Atom)