Ads 468x60px

Friday, December 28, 2012

ADMIN WA MWAKA(KATIKA PAGE)

HII NDIYO ILE KUBWA, Katika hili hatujaangalia admin gani yuko active sana. Ila tumeangalia aliyetufanya tukutane hapa, tuwe pamoja na kuleta mkusanyiko huu.
ADMIN OF THE YEAR niiiiiiiiiiiii DERICK LAWRENCE(Kwa Heshima Kubwa).
Bila Kumsahau Stephen M. Beda(Red Steph) kwa ushauri Mkubwa wa kuendeleza page hii, Na MaAdmin wengine.

PAZIA LA MWAKA 2012 TUMELIFUNGA #GGMU

FAN WA MWAKA, TOP FAN(FACEBOOK PAGE)

* RASHID KILIZA *
HONGERA SANA KWAKE

Mtembelee Facebook RASHID KILIZA

TOP 10 FANS TZ. (FACEBOOK OFFICIAL PAGE)

Haaaya Sasa Huu Ndo Mda!! Hii ni TOP 10 FANS WA MWAKA 2012. Hawa wametoa Mchango wote kwa Pamoja
1. Mohamed Hassan Mazoa
2. Omari Kagawa Bobani
3. Princess Johari De Sagirio
4. Eddy Kudoha
5. Abdul van Mwasha.
6. Gabriel Majaliwa
7. Amos C. Belege
8. Ceaser Mtangi
9. Feed Mkama Paschal
10. WOTE AMBAO HATUJAWATAJA MMETOA MCHANGO MKUBWA
MWAKA 2012
#GGMU

Tuesday, December 25, 2012

MANCHESTER UNITED CHRISTMAS CHALLENGE(ONA VITUKO VYA EVRA NA QUINTONE FORTUNE)

Players vs. Legends vs. Coaches -- all in the name of fun!

Players - Patrice Evra, David De Gea, Darren Fletcher

Coaches - Tony Strudwick, Richard Hawkins, Rene Meuelensteen

Legends - Mickey Thomas, Bryan Robson, Quinton Fortune

Manchester United Christmas Challenge 2012

Saturday, December 22, 2012

Swansea vs Man United-PREVIEW

Viongozi wa ligi weekend hii wanasafiri nje kidogo ya Uingereza,wanaingia nchini Wales kupambana na vijana wanaosadikika kuwa wamechukua sifa ya Arsenal ya kucheza mpira safi na wenye kuvutia,vijana hao sio wengine bali ni Swansea ama ''Swanselona'' kama mashabiki wanavyowaita.
Swansea wamekuwa ni nyoka wenye sumu kali sana hasa wanavyokutana na timu kubwa,wanaongeza umakini kwenye mechi na hayo yoyte yanatetea na mtu mmoja tu,mshambuliaji wao hataaaari asiye na huruma na nyavu MICHU!

Upande wa pili wa shilingi unaowazungumzia wageni ambao ni vinara wa ligi kwa tofauti ya point 6,Man United una sumu kali mara mbili ya hawa wanaoitwa Swanselona.ujio wa Robin Van Persie kutoka Arsenal umeongeza sumu ya United huku akisaidiwa na striker mwenzake mwenye uwezo wa kucheza namba yoyote uwanjani(hata golikipa) Wayne ''Wazzaaa'' Rooney.
Rooney na Van Persie msimu huu wameanza pamoja mara 12 na mechi zote hizo United kashinda zote. Inasadikika pacha yao ndo pacha hatari kwa sasa ligi kuu ukizingatia Robin Van Persie yuko pale juu akiminyana na Michu kwa idadi ya magoli kumi na mbili kila mmoja.

VITU MUHIMU VYA KUZINGATIA KWENYE HII MECHI

*Mara ya mwisho Swansea wanashinda mechi ya nyumbani dhidi ya Man United ilikuwa Januari 1982
*Swansea wamefunga goli moja tu kutoka kwenye mipira iliyokufa msimu huu,mengine yote yaliyobaki 25 wamefunga kwenye mchezo wa pasi
*Hadi sasa Man United magoli yake yamefungwa na wachezaji 15 tofauti
*Man United wanaongoza kwa magoli ya krosi (14) msimu huu na pia wanaongoza kwa magoli ya vichwa(10) msimu huu

WACHEZAJI WA KUWAANGALIA

SWANSEA.
MICHU
Umakini wake na njaa yake ya magoli haufanani na pesa kidogo aliyonunuliwa £2m
Ni hatari sana hasa kama United wataendelea na mchezo wa mabeki wake kujisahau
Ana magoli 12 katika game 17 alizoanza,huku akifunga 6 katika michezo yake 6 ya mwisho

MAN UTD
ROBIN VAN PERSIE

Kwa baadhi ya amshabiki wa United ni kama bado wako kwenye ndoto,hawaamini kama huyu muuaji amekubali kutua Old Trafford kutokea Arsenal,ameisaidia sana na kuitoa Man United shimoni msimu huu
Ni kinara wa magoli pamoja na Michu wote wakiwa na magoli 12 pale juu

MAJERUHI
Man United bado itaendelea kuwakosa Luis Nani,RafaelAnderson,Kagawa huku Vidic akipatikana lakini kuwa na uwezekano mdogo wa kuanza hii mechi. Evans na yeye amepona na kwa taarifa kutoka kwa kocha ni kuwa anaweza kucheza.

Sunday, December 16, 2012

PEP GUARDIOLA NDIYE MTU SAHIHI KWA TIMU YETU

Photo: Kwanini nadhani Manchester United ni nyumbani au panamfaa Pep Guardiola kuliko City,Chelsea au Arsenal!

Katika ulimwengu wa sasa sidhani kama kuna hesabu rahisi kama Kocha Mpya + Chelsea=?
Moja kwa moja jibu ni ''Kufukuzwa wakati wowote'',hesabu zingekuwa hivi tusingekuwa tunafeli wengine hapa!

Baada ya Pep kuachia ngazi Barca na kusema kuwa atapumzika kwa mwaka mzima bila kufundisha Chelsea walitumia mwanya huu kuanza kumtongoza na pesa zao,ukizingatia Pep alishatamka kuwa angefurahi siku kuwafundisha Mata,Oscar na Hazard,Chelsea wakatuma maombi kwa mara ya kwanza,yakagonga mwamba..wakasubiri,huku Pep akiendelea kuifuatilia Chelsea kwa kutia maneno ''Chelsea wamejengeka vizuri sana msimu huu,nimependa walivyoanza'' Na kweli bila hiyana,Chelsea walianza kwa moto sana,lakini ghafla bin vu Di Matteo akatimuliwa,pesa za Abromivich zikamtuma kuwa Pep ndo mtu wa kuja kujaza hiyo nafasi lakini akaumbuka Pesa sio kila kitu,pesa haiwezi kumfanya Messi akacheze Man City na pesa pia haiwezi kumfanya Ferguson astaafu Man United na kwenda China hata kwa £1b kwa mwaka
October Chelsea wakagonga mwamba tena!

KWANINI MAN UNITED KUNAMFAA?

1.Uhakika wa kukaa kazini kwa muda mrefu
Hili halihitaji maelezo,tumeshuhudia Ferguson akaikaa kazini zaidi ya umri wa wengi wetu huku ndani,wangapi walikua wamezaliwa 86??Ferguson ndo anaanza kazi ya United hapo! Sisemi Pep anatafuta team ya kukaa miaka 26,hapana,ila ni mtu anayetaka team itakayompa muda wa kufanya mambo yake! sio kutimuana kama boss na housegirl 

2.Enough resources
Wengi wanaweza kubisha juu ya hili lakini sina maana ya kuwa tuna pesa za kumwaga kama Man City au Chelsea,ndio sisi ni club tajiri lakini hatuna mmiliki tajiri ila kiasi chochote anachotaka kocha anapewa kwa ajili ya maendeleo ya team,hili naomba nithibitishe kwa kauli waliyotoa Glazer Family kuwa Ferguson hata akitaka kumrudisha Ronaldo,pesa iko!!
Kupitia hili ndahani Pep atakuwa na jeuri ya kufanya kazi katika mazingira mazuri pamoja na vitendea azi vya kutosha

3.Barcelona ni kama Man United
Angalia mnavyoshangaa..sijasema tunacheza mchezo wa aina moja(msije mkanitoa roho kwa kuandika uwongo)
Barcelona ni ''football family'' na ndivyo ilivyo wa Man United pia,wiki chache zilizopita Barcelona ilivyocheza na Levante ilikuwa na wachezaji wote 11 kutoka kwenye Academy yao
Man United nasi hatuko mbali sana kwenye hilo,Welbeck,Cleverly,Giggs na Scholes hao ni tunaowajua ila kutokana na takwimu zilizotoka juzi kuwa United ni club ya tano duniani na ya kwanza Uingereza kwa academies bora basi hapa ndo nyumbani kwa Pep. Man City bila ya kumchezesha Miccah Richards basi hawana mchezaji aliyekulia pale,Chelsea nao hivyo hivyo hola!

Baada ya kusema hayo;
Kwanini sio 
Cheslea? Atatimuliwa mapema na hayuko tayari kuchafua CV pale
Man City? Hajazoea kufanya kazi kwenye mazingira ya kifahari hivyo bila kuwa na watu wanaopigania team(wazawa)
Arsenal? Hawana pesa ya kumlipa kama mshara na pia hawatampa kiasi cha kutosha kwenye kununua vitendea kazi

Kwanini Mourinho hawezi kufundisha Man United?
Mtanisamehe kwa hili neno lakini Mourinho ni kocha ''MALAYA''
Ni kocha mzuri sana,japo wengi wetu hatujui kuwa kinachombeba Mourinho ni Man Management na sio skills,ourinho anaweza akakujaza moyo na kukuaminisha kuwa '''bila ya wewe Welbeck Man United Sio Kitu''' ni mzuri sana ila sio wa kukaa sana kwenye club,ndiyo tunahitaji mtu wa kukaa,hatujazoea kubadilisha ovyo,atakuja abebe makombe mawili ya ligi halafu aseme ''I'm looking for Challenges elsewhere''

KUNA MTU YOYOTE ANA MAONI TOFAUTI NA HAYA YANGU KWENYE HILI?NIKO TAYARI KUSAHIHISHWA

(Red Steph)
Kwanini nadhani Manchester United ni nyumbani au panamfaa Pep Guardiola kuliko City,Chelsea au Arsenal!

Katika ulimwengu wa sasa sidhani kama kuna hesabu rahisi kama Kocha Mpya + Chelsea=?
Moja kwa moja jibu ni ''Kufukuzwa wakati wowote'',hesabu zingekuwa hivi tusingekuwa tunafeli wengine hapa!

Baada ya Pep kuachia ngazi Barca na kusema kuwa atapumzika kwa mwaka mzima bila kufundisha Chelsea walitumia mwanya huu kuanza kumtongoza na pesa zao,ukizingatia Pep alishatamka kuwa
angefurahi siku kuwafundisha Mata,Oscar na Hazard,Chelsea wakatuma maombi kwa mara ya kwanza,yakagonga mwamba..wakasubiri,huku Pep akiendelea kuifuatilia Chelsea kwa kutia maneno ''Chelsea wamejengeka vizuri sana msimu huu,nimependa walivyoanza'' Na kweli bila hiyana,Chelsea walianza kwa moto sana,lakini ghafla bin vu Di Matteo akatimuliwa,pesa za Abromivich zikamtuma kuwa Pep ndo mtu wa kuja kujaza hiyo nafasi lakini akaumbuka Pesa sio kila kitu,pesa haiwezi kumfanya Messi akacheze Man City na pesa pia haiwezi kumfanya Ferguson astaafu Man United na kwenda China hata kwa £1b kwa mwaka
October Chelsea wakagonga mwamba tena!

KWANINI MAN UNITED KUNAMFAA?

1.Uhakika wa kukaa kazini kwa muda mrefu
Hili halihitaji maelezo,tumeshuhudia Ferguson akaikaa kazini zaidi ya umri wa wengi wetu huku ndani,wangapi walikua wamezaliwa 86??Ferguson ndo anaanza kazi ya United hapo! Sisemi Pep anatafuta team ya kukaa miaka 26,hapana,ila ni mtu anayetaka team itakayompa muda wa kufanya mambo yake! sio kutimuana kama boss na housegirl

2.Enough resources
Wengi wanaweza kubisha juu ya hili lakini sina maana ya kuwa tuna pesa za kumwaga kama Man City au Chelsea,ndio sisi ni club tajiri lakini hatuna mmiliki tajiri ila kiasi chochote anachotaka kocha anapewa kwa ajili ya maendeleo ya team,hili naomba nithibitishe kwa kauli waliyotoa Glazer Family kuwa Ferguson hata akitaka kumrudisha Ronaldo,pesa iko!!
Kupitia hili ndahani Pep atakuwa na jeuri ya kufanya kazi katika mazingira mazuri pamoja na vitendea azi vya kutosha

3.Barcelona ni kama Man United
Angalia mnavyoshangaa..sijasema tunacheza mchezo wa aina moja(msije mkanitoa roho kwa kuandika uwongo)
Barcelona ni ''football family'' na ndivyo ilivyo wa Man United pia,wiki chache zilizopita Barcelona ilivyocheza na Levante ilikuwa na wachezaji wote 11 kutoka kwenye Academy yao
Man United nasi hatuko mbali sana kwenye hilo,Welbeck,Cleverly,Giggs na Scholes hao ni tunaowajua ila kutokana na takwimu zilizotoka juzi kuwa United ni club ya tano duniani na ya kwanza Uingereza kwa academies bora basi hapa ndo nyumbani kwa Pep. Man City bila ya kumchezesha Miccah Richards basi hawana mchezaji aliyekulia pale,Chelsea nao hivyo hivyo hola!

Baada ya kusema hayo;
Kwanini sio
Cheslea? Atatimuliwa mapema na hayuko tayari kuchafua CV pale
Man City? Hajazoea kufanya kazi kwenye mazingira ya kifahari hivyo bila kuwa na watu wanaopigania team(wazawa)
Arsenal? Hawana pesa ya kumlipa kama mshara na pia hawatampa kiasi cha kutosha kwenye kununua vitendea kazi

Kwanini Mourinho hawezi kufundisha Man United?
Mtanisamehe kwa hili neno lakini Mourinho ni kocha ''MALAYA''
Ni kocha mzuri sana,japo wengi wetu hatujui kuwa kinachombeba Mourinho ni Man Management na sio skills,ourinho anaweza akakujaza moyo na kukuaminisha kuwa '''bila ya wewe Welbeck Man United Sio Kitu''' ni mzuri sana ila sio wa kukaa sana kwenye club,ndiyo tunahitaji mtu wa kukaa,hatujazoea kubadilisha ovyo,atakuja abebe makombe mawili ya ligi halafu aseme ''I'm looking for Challenges elsewhere''

KUNA MTU YOYOTE ANA MAONI TOFAUTI NA HAYA YANGU KWENYE HILI?NIKO TAYARI KUSAHIHISHWA

Saturday, December 8, 2012

DERBY DAY: MATCH PREVIEW

 Pre Match
December 9, 2012
Etihad Stadium — Manchester
Referee:‬ M. Atkinson‎
 
Manchester City - Manchester United Preview: Rivals clash in table-topping tie

Sir Alex Ferguson's side go to the Etihad three points clear of Roberto Mancini's Premier League champions, who will want to pick themselves up after a dismal Champions League exit

HII SI YA KUKOSA: vs MAN CITY @eTIHAD (DERBY DAY)