Ads 468x60px

Saturday, March 29, 2014

DAVID MOYES: "WANANISAPOTI"

Kocha David Moyes amesisitiza sapoti kubwa ya mashabiki wa Manchester United ipo upande wake licha ya kuwepo kwa taarifa kuwa  baadhi ya mashabiki wa United wameandaa bango kubwa linalompinga lililoandikwa maneno "WRONG ONE-MOYES OUT" ambalo litapitishwa na ndege maalum juu ya anga la uwanja wa Old Trafford wakati wa pambano la ligi kuu ya Uingereza ambapo Man United itakuwa ikicheza na Aston Villa.David Moyes
David Moyes pia amesema mashabiki hao wana haki ya kufanya hivyo kutokana na mfululizo wa matokeo mabaya yanayoendelea kuiandama Man United lakini anachoshukuru ni anaungwa mkono na mashabiki wengi, bodi ya klabu na wafanyakazi kwa ujumla.

"Kila mahali ninapoenda ninapata sapoti kubwa kubwa kutoka kwa mashabiki wa Manchester United" Moyes alisema. "Nilikuwa  katika chakula cha jioni jana usiku kwa Darren Fletcher na kulikuwa na wafuasi wengi wa Manchester United ambao walikuja kwangu na kusema, endelea kusonga mbele kwasababu tunaelewa nini hasa tatizo linaloikabili klabu na timu kwa ujumla".

Man United leo kwa mara nyingine itakuwa dimbani Old Trafford kutafuta pointi tatu muhimu dhidi ya timu ngumu ya Aston Villa ili kuona kama utakuwepo uwezekano wa kujisogeza nafasi za juu kusaka nafasi ya kushiriki michuano ya Ulaya msimu ujao.

MECHI NYINGINE ZA EPL ZITAKAZOCHEZWA LEO:

Crystal Palace v Chelsea (saa 12:00 jioni)
Southampton v Newcastle United (saa 12:00 jioni)
Stoke City v Hull City (saa 12:00 jioni)
Swansea City v Norwich City (saa 12:00 jioni)
West Bromwich Albion v Cardiff City (saa 12:00 jioni)
Arsenal v Man City (saa 2:30 usiku)